Mfaransa huyo alikuwa akisubiri kwa hamu kutua Emirates, lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia na fursa ilipomjia tena alikataa na kuwapotezea
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amebainisha kuwa alikaribia kujiunga na Arsenal 2013, lakini alikasirika baada ya klabu hiyo kuacha kumfuatialia.
Griezmann ambaye, alikuwa akicheza Real Sociedad miaka minne iliyopita, alikuwa kivutio kwa Gunners baada ya wakala wa Mfaransa huyo, Eric Olhats, kuwa kwenye mawasiliano na Giles Grimandi wa Arsenal.
Uhamisho huo ulishindikana kukamilika, hata hivyo, Griezmann alijiunga na klabu yake ya sasa Atletico 2014, na mshambuliaji huyo ameeleza jinisi alivyoitosa Arsenal baada ya kuona klabu nyingine zinahitaji huduma yake.
"Nilisubiri, nikasubiri na kusubiri," Griezmann aliandika kwenye ukurasa wake mpya. "Kulipokuwa hamna habari, Eric alimpigia Grimandi, ambaye alisema kuwa bado meneja alikuwa akivutiwa na mimi na tukaendelea kusubiri.
"Hatimaye, saa chache kabla ya soko kufungwa, alitufahamisha kuwa Arsenal haiwezi kukamilisha usajili. Sipendi kuambiwa jambo alafu lisitokee.
"Kwa hiyo, Eric aliniambia baadaye kuwa klabu hiyo ya London ilikuwa ikitamani huduma yangu tena, nilimwambia 'chana nao, baada ya kutuangusha'".
Griezmann alifunga mara mbili timu yake iliposhinda 5-0 dhidi ya Levante wikiendi iliyopita, matokeo mazuri kufuatia ushindi mwingine wa Atletico wa 2-0 dhidi ya Roma.
Maoni
Chapisha Maoni