Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

Madrid na PSG katika vita kumuwania Dybala. Allegri kutimkia PSG.

Klabu za Real Madrid na PSG zinavutiwa na mshambuliaji wa Juventus  Paulo Dybala. Mtazamo wa Argentina unaonekana kama mbadala ya Neymar kwa vilabu vyote viwili. Zaidi ya hayo, Juventus haina kipingamizi katika kumuuza Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 24 na tayari imemtaja Isco kama mbadala wa nafasi hiyo. Pia PSG wanamuona kocha wa Juventus Massimiliano Allegri kama mbadala wa kocha wao ambaye hakuwa na matokeo mazuri hivi karibuni katika ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya miamba ya soka ya Hispania Real Madrid, Unai Emery. Japo kocha wa zamani wa Barcelona Lois Enrique alikuwa katika nafasi ya juu kabisa ya vigogo hao lakini kuja tetesi huenda akatimkia England.

Tottenham 3 Swansea 0, Nusu fainali kombe la FA.

Christian Eriksen aliifungia mara mbili Tottenham na kuisaidia timu yake kutinga fainali za Kombe la FA kwa msimu wa pili mfululizo katika Uwanja wa Liberty dhidi ya Swansea. Magoli ya kipindi cha kwa ya Eriksen na Erik Lamela yameweka Spurs kwenye njia nzuri ya kushinda taji lao la tisa la FA. Katika kipindi cha pili Eriksen alihitimisha karamu hio ya ushindi kwa kufunga goli katika dakika ya 62 ya mchezo. Spurs wanatafuta taji la kwanza tangu waliposhinda Kombe la Ligi ya 2008.

Ramos na rekodi ya ukorofi.

Wakati wakina Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanashindana kuweka rekodi za mabao na kufanya mambo mazuri katika soka, hali ni tofauti kwa mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos kwani anaweka rekodi za kihuni. Rekodi zinaonesha Ramos ndio beki ambaye anacheza rafu mbaya zaidi katika ligi ya soka nchini Hispania La Liga suala ambalo limewalazimu waamuzi katika ligi hiyo kumpa kadi nyekundu 19. Hakuna mchezaji yeyote tangu La Liga ianze ambaye amewahi kupewa kadi nyekundu kama ambavyo Sergio Ramos amepewa na ndio anashikilia rekodi ya kadi nyingi nyekundu katika michuano hiyo. Ukiacha ufalme huo wa kadi alionao Ramos katika La Liga, sehemu pekee ambayo Ramos alikuwa amebakisha ni Champions League ambako huko Paul Scholes ndio alikuwa akishikilia rekodi ya kadi za njano akiwa na 36. Lakini sasa Ramos amekaa juu ya Scholes kwani baada ya mchezo vs PSG sasa Ramos anakuwa na jumla ya kadi za njano 37 idadi ambayo hakuna mchezaji yeyote Champions League ambaye amewahi kupewa kadi nying...

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...

Bado mechi 12 La Liga imalizike, Madrid kupigania nafasi ya 4.

Jana Real Madrid waliifuata Espanyol katika moja ya michezo ambayo imewashtua watu, Real Madrid walikufabao moja dakika za lala salama goli likiwekwa kimiani na Gerrard Moreno katika dakika ya 92. Pamoja na Gareth Bale kufikisha michezo 116 katika ligi kuu nchini Hispania idadi ambayo inamfanya kuwa sawa na David Beckham kama Waingereza waliocheza michezo mingi La Liga lakini haikuwa siku nzuri kwao. Real Madrid sasa wanakuwa na alama 51 ambazo wanakuwa wamezipata katika michezo 26(mchezo mmoja zaidi ya walioko nafasi ya nne), huku Valencia wenyewe wakiwa na alama 49 na mchezo mkononi. Kwa Madrid ina maana kwamba wamebakisha michezo 12 tu sawa na alama 36 ili kumaliza msimu lakini presha kubwa kwao ni namna walivyopishana na timu ya 4 na hii inawatisha kufika katika nafasi hiyo. Kwa macho ya kawaida inaonekana Madrid msimu huu wanaweza kupigania nafasi ya nne kwani ndoto za ubingwa zimeshakufa na Champions League ndio sehemu pekee kwao kuweka heshima msimu huu.

Tetesi za soka Ulaya na Alhamisi Machi 1 2017

West Ham iko tayari kumsiani mlinzi wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kwa paundi milioni tatu kutoka kwa West Brom ikifika mwisho wa msimu. (Birmingham Mail) Kiungo wa Arsenal na timu ya England, Jack Wilshere, 26 anasema atatoka kwenye klabu hiyo kati kati ya mwaka huu, wasipo mpatia mkataba bora zaidi. (Sun) Manchester United kuachana na mipango ya kuupanua uwanja wa Old Trafford mwaka huu na kujikita zaidi katika kumuunga mkono Jose Mourinho katika kutafuta wachezaji.(Mail) Winga wa Chelsea kutoka Brazil,Willian,29, anaweza iacha Stamford Bridge katikati ya mwaka na huenda akujiunga na timu ya AC Milan au Manchester United (Star) Manchester United wameuongeza muda ya mikataba ya viungo Ashley Young, 32, na Daley Blind, 27, na ule wa mlinda mlango Sam Johnstone, 24 Mashetani hao wekundu wana waacha viungo Marouane Fellaini, 30, na Michael Carrick, 36, na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambao watakuwa huru kuondoka na kwa usajili huru majira ya joto. Alan Pardew atafukuzwa k...

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)