Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 31 December 2017

Manchester United wanafuatilia kwa karibu ripoti za tofauti baina ya Cristiano Ronaldo na viongozi wa Real Madrid, kimedai Mirror . Magazeti yanasema kuwa uhusiano baina ya Ronaldo na Florentino Perez umevunjika, jambo linaloleta shaka juu ya mustakabali wake Bernabeu Philippe Coutinho anaelekea kuwa mchezaji ghali zaidi kuuzwa Ligi Kuu Uingereza katika historia akitarajiwa kutua Barcelona kwa kitita cha £125 milioni, kwa mujibu wa Express . Mbrazili huyo alikuwa shabaha ya Barca miezi mingi, lakini Blaugrana walishindwa kufikia makubaliano na Liverpool majira ya joto. Nyota wa Inter Joao Mario ameingia kwenye arada za Manchester United wakitaka kumsajili kuziba pengo la Henrikh Mkhitaryan, kwa mujibu wa Sun . Hali si shwari kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Armenia katika Old Trafford, na klabu nyingi zinaitaka saini yake. Ikiwa atatimkia Serie A, United watafanya jaribio la kumsajili Mreno wa Nerazzurri kwa kiasi cha paundi milioni 40. Real Madrid wanafikiria kumsajili beki ...

Sanchez anauzwa 35 million tu.

HAYA! Alexis Sanchez huyo hapo, mchukueni! Arsenal imesema hivi, staa huyo wa Chile atakuwa huru tu kwenda kwenye timu yoyote anayotaka kama tu itawekwa Pauni 35 milioni mezani. Kwa lugha nyepesi tu. Arsenal inampiga bei staa wake huyo kwa Pauni 35 milioni. Ndiyo, Pauni Thelathini na Tano milioni tu. Sanchez aligomewa kwenda Manchester City kwenye dirisha lililopita na kocha Arsene Wenger alidai kwamba hamuuzi kwenye dirisha la Januari, lakini kwa sasa anaonekana kuanza kulegeza masharti. Kwa sababu mkataba wa mchezaji huyo utafika tamati mwisho wa msimu na kwamba ataondoka bure, Arsenal kwa sasa wamemua ni heri wakaambulia chochote kuliko kumshuhudia mchezaji huyo mahiri kabisa kuondoka bila ya kupata chochote. Kutangazwa kwa dau hilo kuna maana kwamba sasa Manchester City, Paris Saint-Germain, Bayern Munich na timu nyingine zinazohitaji huduma yake ni wakati wao tu kuanza kupeleka ofa zao kwa ajili ya kupata huduma yake. Mchezaji mwenyewe anataka kuachana na Arsenal kwa haraka i...

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 29 December 2017

Njia itakuwa nyeupe kwa Barcelona kumsajili Antoine Griezmann kwa kitita cha paundi £89 milioni kwani Manchester United hawatafanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid kwa mujibu wa Marca . Barcelona bado inataka kumsajili Angel Di Maria, na Paris Saint-Germain imetaja bei yake kuwa £45 milioni kwa mujibu wa ESPN .Mwargentina huyo si mchezaji muhimu sana kwa PSG tangu ujio wa Neymar na Kylian Mbappe. Tottenham wamedhamiria kusambaratisha bajeti yao ili kuweza kumbakisha Harry Kane kwenye klabu yao, kwa mujibu wa Daily Mail . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa kinara wa mabao 2017 akifunga magoli 56, kwa sasa analipwa £110,000 kwa wiki kiasi ambacho ni kidogo kwa wachezaji wa kaliba yake. Mshahara wa Kane utakuwa unaongezeka kwa mara ya nne tangu Agosti 2014, Spurs wakilenga kuzipindua ofa za Real Madrid. Klabu za Uingereza zimepata fununu kuwa huenda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anaweza kumruhusu kuondoka winga wake Yanni...

Dembele kuikosa El classico

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa Ousmane Dembele hatacheza mechi ya Clasico wikiendi ijayo licha ya kuanza mazoezi Dembele hajacheza tangu alipopata majeraha dhidi ya Getafe Septemba, na kulazimika kukaa nje kwa miezi. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa Kifaransa amerejea kwenye ratiba ya mazoezi, na kuamsha tetesi kuwa anaweza kuwemo kwenye safari ya kwenda Real Madrid Desemba 23. Lakini Valverde amesema Dembele hatarejea kibaruani hadi Januari, akisisitza kuwa hakuna haja ya kumuingiza mchezaji huyo matatizoni. "Amefanya mengi kwenye mazoezi wiki hii, lakini hajakamilisha mazoezi kamili hadi sasa," kocha aliwaambia waandishi Jumamosi. "Wiki ijayo tutamwongezea kazi, lakini mpango ni ule ule wa awali. Januari ndio tunamtarajia kurudi dimbani. "Itakuwa mapema - na tutamweka matatizoni kumchezesha mapema. Malengo yetu ni kumwacha kwanza hadi Januari." Kabla ya safari kwenda Bernabeu kwa mechi ya kwanza ya Clasico kwa msimu huu, wataikaribisha...

Manchester City wailaza Tottenham 4-1

Magoli kutoka kwa Ilkay Gundogan, Kevin De Bruyne na mawili kutoka kwa Raheem Sterling yaliipatia Man City ushindi wa 4-1 dhidi ya Tottenham Gundogan alifunga goli la kwanza kwa kichwa akiunganisha kona ya Leroy Sane dakika 14 baada ya wenyeji kuumiliki mpira dhidi ya Spurs na waliendelea kutawala mchezo. Shuti la De Bruyne liliwavunja nguvu Spurs baada ya mpira kuzama wavuni na Sterling aliweka kimiani mara mbili kwa shuti la karibu baada ya kukosa goli la wazi kufuatia Gabriel Jesus kukosa penalti ambayo iligonga mwamba. Chrstian Eriksen aliipatia Spurs goli la kufutia machozi dakika za mwisho lakini pengo lao dhidi ya vinara hao wa ligi limeongezeka hadi pointi 21. City wameshawafunga mahasimu wao wote wa taji Ligi Kuu Uingereza msimu huu na mbio zao kuelekea ubingwa wa Uingereza zinaonekana kukosa mpizani. Walifunga goli lao la kwanza kupitia nafasi yao ya pili, Baada ya Gundogan kuwahadaa mabeki wa Spurs na waliruhusu goli kirahisi mno kupitia Raheem Sterling aliyetupia goli ...

Eric Baily nje miezi mitatu

Beki wa Manchester United Eric Bailly atafanyiwa upasuajiwa kifundo cha mguu na kukaa nje miezi mitatu Bosi wa United Jose Mourinho alisema katikati ya juma kuwa beki huyo wa kati atapigwa kisu kurekebisha tatizolae, na amethibitisha Ijumaa kuwa hofu yake imedhihiri. "Anakwenda kufanyiwa upasuaji, uamuzi umefanyika," Mourinho alisema. "Sisemi kwamba yupo nje kwa muda wote wa msimu, lakini kwa miezi mitatu ijayo." Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Bailly amekosa mechi nane mfululizo, na mechi ya karibuni aliyocheza ni ile waliyofungwa 1-0 na Chelsea November 5 . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipata majeraha kwenye majukumu ya kimataifa lakini Mourinho alisema mapema juma hili kuwa anaridhishwa na wanaoweza kuziba pengo lake. Alisema: "Nimemchezesha [Chris] Smalling na [Phil] Jones na tunaye [Victor] Lindelof na [Daley] Blind kwenye benchi. Marcos Rojo alipata majeraha [dhidi ya Manchester City] lakini tatizo si kubwa. "Katika msimu wote, ...

Mourinho atakiwa kutoa ufafanuzi wa maneno yake.

FA imemuuliza meneja wa Manchester United kuelezea kauli zake alizosema kabla ya mechi ya Ligi Kuu Uingereza dhidi ya City uwanjawa Old Trafford Jose Mourinho ametakiwa na Shirikisho la Soka kuelezea kauli alizosema kwenye vyombo vya habari kabla ya mechi kubwa ya Manchester. Mreno huyo alishuhudia timu yake Manchester United ikinyukwa 2-1 na mahasimu wao Manchester City kwenye mechi ya Ligi Kuu Uingereza Jumapili ambapo baada ya mechi kulikuwa na tafrani nyingi kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo Old Trafford. FA tayari imeshaziuliza klabu zte kuhusu mtazamo wao katika tukio hilo, ambapo kwa mujibu wa habari Mourinho alimwagiwa maziwa. Hata hivyo Mourinho amejikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kauli zake alizosema kabla ya mechi, alipoishutumu City kwa kutumia ujanja kwenye mchezo, akisema: "Wakipulizwa kidogo na upepe wanaanguka." Mourinho pia alidai kuwa City wanatumia "mbinu ya faulo" kuvuruga mchezo alipokuwa akizungumzia mechi dhidi ya hasimu wake wa...

Wenger: Manchester united hawajaonyesha nia ya kumtaka Ozil

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa Manchester United hawajawasiliana na Gunners kuhusu uhamisho wa Mesut Ozil. Kiungo huyo akiwa amebakiwana miezi sita tu kwenye mkataba wake, klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na United zimehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Mjerumani huyo. Hata hivyo, akidai kuwa hana uhakika kuhusu maendeleo ya mazungumzo na Ozil, Wenger amesisitiza kuwa kiungo huyo hataondoka London Kaskazini kabla ya mwisho wa msimu. Mfaransa huyo aliwaambia waandishi: "Karibu kiasi gani? Sijui ni karibu kiasi gani. Man United hawajawahi kutupigia, kwa hiyo sijui jambo hilo limekujaje. "Hilo ni jambo ambalo limezushwa. [Atabaki] hadi mwisho wa msimu, mengine yapo wazi." Pamoja na kuwa Ozil amefunga magoli mawili na sare tano katika mechi 14 Ligi Kuu Uingereza msimu huu, hajafanikiwa kufunga katika mechi tatu za mwisho.

David Silva ni zaidi ya kiungo

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amemwelezea David Silva kama kiungo aliyekamilika baada ya kufunga magoli katika mechi za hivi karibuni. Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania ameweka kimiani katika ushindi mwembamba dhidi ya West Ham United na Manchester United kwenye mechi zilizopita, kadhalika mabao mawili aliyofunga dhidi ya Swansea City Jumatano. Guardiola amemsifia Silva kufuatia kiwango chake maridadi, akidai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 sasa ni "mnyama" anapokuwa akiwinda goli mbele ya lango. "Ana kila kitu, hasa anapokuwa dhidi ya wapinzani wakuu." alikiambia BBC Sport. "Kila mmoja anazungumzia ufundi wake, hakuna shaka katika hilo. Hata kipofu anaweza kuona. "Lakini huwezi kufikiri ni kiasi gani alivyo mahiri dhidi ya wapinzani. Anaonekana kama mtu wa aina tofauti lakini, wow, ni mnyama katika kipengele cha kushinda mech. "Mara zote tumekuwa tukizungumzia hilo: 'Unahitaji kufunga magoli, David. Unaweza kufanya ...

Bakayoko anahitaji msaada

Bakayoko ameshindwa kuonyesha kile kilichotarajiwa kutoka kwake ingawa mchango wake kwenye timu bado ni muhimu, na Kante amemba Mfaransa huyo asaidiwe Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante amesema kuwa timu yake ina jukumu la kumsaidia mchezaji mwenzao Tiemoue Bakayoko anapoendelea kuzoea maisha ya Ligi Kuu Uingereza. Mfaransa Bakayoko, anahangaika kuonyesha tofauti Chelsea tangu atue London akitokea Monaco kwa £40m, alitolewa kipindi cha pili klabu hiyo ikifungwa 1-0 na West Ham Jumamosi

16 bora: Chelsea VS Barcelona

Chelsea wamepangwa kukutana na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa. Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United wakutana na Sevilla wanaocheza La Liga nao Liverpool wakutane na FC Porto ya Ureno. Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Paris St-Germain. Klabu tano kutoka England zilifuzu kwa hatua ya makundi msimu huu, ambayo ni rekodi. Chelsea ndio pekee wa Uingereza waliofuzu wakiwa wa pili kutoka kundi lao, klabu nyingine zote zilimaliza kileleni Washindi wa makundi watakuwa ugenini mechi za kwanza 13/14 na 20/21 Februari na nyumbani mechi za marudiano mbamo 6/7 na 13/14 Machi. Fainali itachezewa Kiev mnamo 26 Mei. Droo kamili: Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Yanga: Hatuvunji mkataba na Ngoma

Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema pamoja na malumbano yote na mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma lakini haitavunja mkataba naye. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara Hussein Nyika, amesema matatizo yaliyotokea Kati Yao na Ngoma ni ya kawaida ambayo wanaweza kukaa mezani na kuyamaliZa hivyo hawana mpango wa kuachana na mchezaji huo. "Maneno yamekuwa mengi kwenye vyombo vya Habari kuhusu kupishana kwetu na Ngoma kitu cha msingi hapa ambacho naweza kuwaeleza wale watu w anaotaka tuachane na Ngoma hilo halitotokea tutakaa chini chini kuyazungumza na hatimaye kuyamaliza," amesema Nyika. Kiongozi huyo amesema anajua kwamba wanao paisha jambo hilo ni wapinzani wao Simba ambao lengo lao ni kumchukua mchezaji huyo na hilo halitowezakana kutokana na kushtukia mpango wao. Ngoma alingia kwenye mgogoro n uongozi was timu yake baada ya kujiamlia kwenda kwao Zimbabwe kujiuguza bila ruhusa kutoka kwa viongozi wa timi na uongozi ...

Azam Fc: Sisi ndiyo mabingwa

Azam FC imejiwekea malengo ya kufika fainali ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) ikiwemo kulitwaa taji hilo msimu huu ambalo linatetewa na Simba. Kauli hiyo ameitoa Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Idd Nassor Cheche, wakati akizungumzia droo ya michuano hiyo iliyotolewa juzi ikishuhudiwa wakipangwa kuanza na Area C United ya Dodoma, amedai kuwa wameipokea vizuri ratiba hiyo na watajipanga kufanya kweli. “Sisi malengo yetu ni kufika fainali na tuchukue kombe, kwa hiyo kila mtu tutakayepangiwa naye tunajidhatiti, tunajiandaa vizuri ili tuhakikishe ile dhamira yetu inafikia malengo,” alisema Cheche. Kocha huyo wa muda mrefu ndani ya Azam FC akianzia majukumu ya kuwa Kocha Mkuu kwenye timu ya vijana (Azam U-20) kabla ya kuteuliwa kuwa Kocha Msaidizi Desemba mwaka jana akiwa chini ya Mromania Aristica Cioaba, alisema kuwa wamejipanga vema msimu huu tofauti na mwaka jana. “Mwaka huu tumejipanga vizuri zaidi tofauti na mwaka jana na tunaari na wachezaji wanaari na tum...

Huenda Msuva akaivaa Yanga

Utamu wa vita ni kumjua adui yako, Yanga inajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza mwakani mmoja wa wapinzani wake katika kusaka taji hilo ni mshambuliaji wake wa zamani, Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadidi ya Morocco. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linataraji kutangaza ratiba ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika Jumatano ijayo Desemba 13 jijini Cairo, Misri kwa michuano hiyo itakayoanza mwanzoni mwa Februari na kumalizi Novemba mwakani bingwa atajinyakulia dola 2.5 milioni. Yanga chini ya kocha, George Lwandamina imedhamiria kufanya vizuri katika michuano hiyo na tayari imeanza kufanya usajili wachezaji mbalimbali wa kimataifa ili kutimiza lengo hilo. Mabingwa hao wa Tanzania Bara, Yanga itaanza Ligi ya Mabingwa hatua ya awali kama ilivyokuwa kwa Difaa El Jadidi inayoshiriki mashindano hayo kwa mara kwanza tangu 2010 ilipotolewa katika raundi ya kwanza. Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani hatua ya makundi itashirikisha timu 16,...

Majogoo ya jiji kuwavaa Everton

England. Liverpool watakuwa nyumbani huko Anfield leo kuwakaribisha Everton mechi itakayopigwa saa kumi na moja na robo (11:15 jioni). Timu hizo zinakwenda kwenye mechi hiyo kila moja ikiwa katika hali nzuri baada ya kushinda mechi zao zilizopita, ambapo Everton ilishinda mabao matatu ugenini kwenye Europa League, huku Liverpool ikimpiga mtu mabao saba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mechi nyingine ya leo, Arsenal iliyoshinda BATE 6-0 watakuwa na shughuli pevu ugenini kwa Southampton.

Hakuna kupaki basi

London, England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewataka wachezaji wake kuepuka mipira ya adhabu karibu na goli lao na kutopaki basi wakati watakapowakabili watani zao wa jadi Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford leo Jumapili. Guardiola amewaonya wachezaji wake kuacha kutengeneza mazingira ya mipira ya adhabu katika mchezo huo muhimu zaidi kwao. Kocha huyo Mhispania, anahofia Man United inaweza kupata mabao kupitia mipira ya adhabu endapo Man City haitakuwa makini. Man United ina wachezaji wengi warefu kulinganisha na Man City. Romelu Lukaku, Nemanja Matic, Chris Smalling na Zlatan Ibrahimovic ni wachezaji warefu ambao watakuwa tishio kwa Man City. Kiungo wa pembeni aliyerudishwa kucheza beki wa kushoto Ashley Young amepata umaarufu kwa mashuti ya mpira wa adhabu. Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya bilioni moja watakuwa wakitazama pambano la Manchester United dhidi ya Manchester City. Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ataukosa mchezo huo akitumikia adhabu y...

Tetesi za soka Ulaya

Manchester United itafanya mchakato kumsajili kiungo wa Real Madrid Marco Asensio dirisha la uhamisho la Januari baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale, kwa mujibu wa Don Balon . Mashetani Wekundu wanajiamini watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo wa miaka 21 kwani ameshindwa kupata nafasi ya kudumu Santiago Bernabeu. Manchester United wapo tayari kusikiliza ofa kuwauza mabeki wao Luke Shaw na Matteo Darmian, kwa mujibu wa The Daily Record . Shaw ambaye amesumbuliwa na majeraha amepewa nafasi kujiunga na klabu nyingi za Uingereza wakati Muitaliano Darmian hatakiwi kwenye kikosi cha Jose Mourinho. United wanataka kutunisha mfuko wao ili kuwasajili beki wa kushoto Alex Sandro na Danny Rose majira ya baridi. Real Betis wanaandaa ofa kumsajili Daniel Sturridge kutoka Liverpool, kwa mujibu wa El Gol Digital . Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akihaha kutafuta muda wa kucheza zaidi Anfield na atapewa nafasi kutimkia Hispania Januari. Chelsea wapo tayari kutoa...

Tetesi za soka Ulaya

Everton wanajipanga kutoa dau la £60 milioni kwa ajili ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, kimedai Mirror . Toffees wamekuwa kwenye wakati mgumu msimu huu baada ya kushindwa kuziba pengo la mshambuliaji wa kati Romelu Lukaku. Inter wapo tayari kupigana vikumbo na Juventus kwa ajili ya saini ya mchezaji wa Liverpool Emre Can, kwa mujibu wa Tuttosport . Kiungo huyo atakuwa amemaliza mkataba wake Anfield mwisho wa msimu huu na alikuwa karibu kutua Turin majira ya joto. Real Madrid wamewasiliana na mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard kuangalia uwezekano wa kumleta Mbelgiji huyo Hispania kwa mujibu wa Diario Gol . Mchezaji huyo anasita kusaini mkataba mpya Stamford Bridge na ameeleza jinsi anavyoihusudu Real Madrid. Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Schalke Leon Goretzka na watampata kama mchezaji huru, kwa mujibu wa The Sun . Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani atakuwa amemaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu na yupo huru ku...

Mourinho ni pacha wangu

Wawili hao wataendeleza uhasimu wao katika Old Trafford Jumapili mchana City watakapoikabili Manchester United katika mechi ya vinara wa ligi Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa yeye na Jose Mourinho ni 'kama mapacha' kutokan na shauku zao kutwaa mataji. Wawili hao wataendeleza uhasimu wao katika Old Trafford Jumapili mchana City watakapoikabili Manchester United katika mechi ya vinara wa ligi. Guardiola na Mourinho hawajawahi kutazamana machoni, mara ya kwanza wakianza wakiwa Hispania Barcelona na Real Madrid, lakini kocha huyo wa City amesema wanafanana kuliko watu wanavyodhani. Alipoulizwa kama Mourinho naye amedhamiria kutwaa mataji, Guardiola aliwaambia waandishi: "Kabisa! Katika hilo sisi ni mapacha. Anataka kushinda mataji, Nataka kushinda mataji. "Antonio Conte kama ilivyo kwa Jurgen Klopp na Mauricio [Pochettino]. Tunapenda kushindana, tunapenda kushinda mechi lakini amini maneno yangu, wala si jambo la kipekee kwetu kuzifunga timu za Mo...

Hazard atamani kutua Madrid

Mazungumzo baina ya Chelsea na Eden Hazard kwa ajili ya mkataba mpya yamesimama kwani Mbelgiji huyo anataka kutimkia Real Madrid kwa mujibu wa The Times . Imeripotiwa kuwa Blues wapo tayari kumfanya Hazard kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, kwa mshahara wa £300,000 kwa wiki. Lakini Hazard anasita kuongeza mkataba na bado amebakiwa na miaka miwili na nusu kwani anahofu kukosa kutimiza ndoto ya kujiunga na Los Blancos. Rais wa Real Madrid Florentino Perez anafikiria kumtoa Toni Kroos kwa Juventus ili ampate Paulo Dybala kama biashara ya kubadilishana, kwa mujibu wa Rai Sport . Thibaut Courtois ataruhusiwa kuondoka kama mchezaji huru Chelsea ifikapo 2019 kwani Mbelgiji huyo ameendeea kukataa kusaini mkataba mpya kwa mujibu wa, The Sun . Ikiwa Blues watashindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mlinda mlango huyo - ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Real Madrid - atalazimika kumaliza mkataba wake badala ya kumuuza kabla ya kuumaliza mkataba. M...

Urusi kutoshiriki michuano ya Olimpiki

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, imeifungia nchi ya urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani. Rais wa IOC Thomas Bach na bodi yake walitangaza adhabu hiyo jana jioni baada ya kukutana katika mji wa Lausanne nchini Switzerland, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba. Serikali ya Urusi ilihusika katika udanganyifu wa kuanda michuano ya olimpiki iliyofanyika nchini humo mwaka 2014 pamoja na udanganyifu kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni. Uchunguzi huo ulikuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa IOC Samuel Schmid, Licha adhabu hiyo wanariadha wa Urusi wanaweza shiriki michuano ya majira ya baridi kama wanaridha huru ambao watakuwa wakiwakilisha nchi.

Ghoulam na Napoli hadi 2022

Beki wa kimataifa wa Algeria anayekipiga na klabu ya Napoli, Faouzi Ghoulam ameongeza mkataba na klabu yake utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2022. Mkataba wa sasa wa mlinzi huyo unamalizika tarehe 30 ya mwezi june mwaka 2018, hivyo mkataba mpya umeongeza miaka minne ya wa kukipiga na vinara wa Seria A. Ghoulam kwa sasa anauguza jeraha la goti alilofanyiwa upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Manchester City. Beki huyo alijiunga na Napoli mwaka 2014, akitokea Saint Etienne ya nchini Ufaransa na amekwisha cheza michezo 153 katika kablu hiyo