Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amevaa Ribbon ya njano wakati wa fainali za Carabao Cup dhidi ya Arsenal, licha ya kushtakiwa na Chama cha Soka. Kocha wa Kikatalani alishtakiwa na FA siku ya Ijumaa, siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal, kwa kuvaa Ribbon, ambayo ni ishara ya msaada kwa wanaharakati wa uhuru wa Kikatalani. Kuvaa Ribbon ya njano ni kuonekana na chama kuwa kinyume na kanuni zake kwa sababu sheria zake dhidi ya Siasa katika mpira . Ribbon huvaliwa na wale wanaoelewa na shida ya wanaharakati wa uhuru wa Kikatalani Jordi Sanchez na Jordi Cuixart, ambao walikuwa wamefungwa kwa harakati zao katika katika kushinikiza uhuru wa Kikatalani.