Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2017

Yanga dhidi ya Ngoma

Yanga imechoshwa na visa na vituko vya mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma na sasa inapanga namna ya kumwajibisha Klabu Yanga imepanga kumuwajibisha mshambuliaji wake raia wa Zambabwe Donald Ngoma, kwa kosa la kwenda kwao bila ruhusu ya klabu hiyo ambayo anaitumikia kwa msimu wa tatu sasa. Chanzo cha bari kutoka ndani ya klabu hiyo kimeiambia Goal , kuwa uongozi wa juu upo katika mjadala wakijadili namna ya kumwadhibu mchezaji huyo ambaye hajaichezea timu yao kwa miezi miwili baada ya kutimkia kwao Zimbabwe bila ruhusa ya klabu. "Tupo kwenye kikao cha kumjadili Ngoma, amekuja jana kutoka kwao Zimbabwe tunachotaka ni kutuambia nani alimpa ruhusa ya kwenda kwao na kingine tunataka kujua kama anataka kucheza Yanga au kuondoka maana tunashindwa kumuelewa kwa yale anayotufanyia," imesema taarifa hiyo. Chanzo hicho kimedai pamoja na majeruhi aliyokuwa nayo mchezaji huyo lakini alipaswa kubaki nchini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu kama ilivyo kwa wenzake wawili Amissi Tamb...

ANTOINE GRIEZMANN: "NIMEKUWA NIKISUBIRI KUHAMIA ARSENAL"

Mfaransa huyo alikuwa akisubiri kwa hamu kutua Emirates, lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia na fursa ilipomjia tena alikataa na kuwapotezea Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amebainisha kuwa alikaribia kujiunga na Arsenal 2013, lakini alikasirika baada ya klabu hiyo kuacha kumfuatialia. Griezmann ambaye, alikuwa akicheza Real Sociedad miaka minne iliyopita, alikuwa kivutio kwa Gunners baada ya wakala wa Mfaransa huyo, Eric Olhats, kuwa kwenye mawasiliano na Giles Grimandi wa Arsenal. Uhamisho huo ulishindikana kukamilika, hata hivyo, Griezmann alijiunga na klabu yake ya sasa Atletico 2014, na mshambuliaji huyo ameeleza jinisi alivyoitosa Arsenal baada ya kuona klabu nyingine zinahitaji huduma yake. "Nilisubiri, nikasubiri na kusubiri," Griezmann aliandika kwenye ukurasa wake mpya. "Kulipokuwa hamna habari, Eric alimpigia Grimandi, ambaye alisema kuwa bado meneja alikuwa akivutiwa na mimi na tukaendelea kusubiri. "Hatimaye, saa chache kab...

Mwaka mmoja sasa.

Ni mwaka mmoja umepita tangu kutokea kwa ajali mbaya ya ndege ambayo iliwahuzunisha wanamichezo kote duniani iliyohusisha wachezaji wa timu ya Chapecoence ya nchini Brazil.

Walazimisha Coutinho atue Barcelona.

     Wachezaji wa timu ya Fc Barcelona akiwemo Lionel Messi, wametuma maombi kwa rais wa Klabu hiyo amsajili mchezaji wa Liverpool Philippe Coutinho katika usajili wa majira ya baridi Januari.   Klabu hiyo ya Catalan ilijaribu kumsajili mchezaji huyo katika dirisha la usajili lililopita lakini Liverpool walisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi. Bei inayotabiriwa ni €133 million lakini inaweza kuwa zaidi ya hapo

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 29th Nov 2017

Real Madrid wanalenga kumsajili beki wa Chelsea na Brazil David Luiz 30 ambaye hatakikani katika uwanja wa Stamford Bridge msimu huu. (Daily Mail) Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa hajaelezwa iwapo atalazimika kuwasajili wachezaji wowote katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari iwapo mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kuwafikia viongozi wa ligi Manchester City. (Guardian) Mchezaji wa Manchester City na raia wa Ujerumani mwenye umri wa 21 Leroy Sane atapewa kandarasi mpya na Manchester City mwishoni mwa msimu huu. (Sun) Watford wameonya kwamba mshambuliaji wao raia wa Brazil Richarlison, 20, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Fluminence mnamo mwezi Agosti kwa kitita cha £11m na anavutia klabu za Tottenham na Chelsea hauzwi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (London Evening Standard) Chelsea wanatarajiwa kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro ,26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil mwak...

''Lukaku alihitaji marufuku kwa kumpiga teke mwenzake''

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku alifaa kupewa marufuku kwa kumpiga teke mlinzi wa Brighton Gaetan Bong, mchanganuzi wa maswala ya soka wa BBC Ian Wright amesema. Kisa hicho kilitokea wakati klabu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0 siku ya Jumamosi, lakini hakuonekana na refa Neil Swarbrick. Jopo la shirikisho la soka nchini humo liliamua kwamba hafai kuchukuliwa hatua yoyote. ''Iwapo wataangalia tena, kwa nini wasione kwamba kilichofanyika kilikuwa makosa anafaa kuadhibiwa? Ndio'', Wright aliambia BBC Radio 5 live. ''Mara nilipoona nidhani wataingalia mara ya pili. Unafikiria ni kwa nini ameepuka''?

Tetesi za usajili Ulaya

Miamba ya soka kutoka London, Chelsea wako mbioni kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang ambaye anaonekana kutokuwa na moyo wa kuichezea klabu hiyo tena. Klabu ya Borussia Dortmund imeziarifu baadhi ya timu kuwa atakuwa sokoni Januari mwakani. Klabu za Arsenal na Liverpool ziko katika upinzani wa kumnyakua winga wa PSG Julian Drexler. Liverpool wamekuwa wakimuhitaji winga huyo kwa mkopo lakini PSG wamesisitiza kuwa anauza. Pia ikumbukwe kabla ya Draxler kwenda PSG alikuwa akihitajika na washika bunduki wa London. Pia klabu ya FC Barcelona bado wanajiandaa kumnasa kiungo wa klabu ya Tottenham katika dirisha dogo la usajili. Miamba hiyo inaami kuwa anaweza kuwa mbadala wa Andres Iniesta ambaye soka lake linaelekea ukingoni. PSG wako mbele Manchester City katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez ambaye ana kila dalili za kuondoka klabuni hapo Januari mwakani. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Chile unafikia ukomo mwakani Ja...

Maajabu ya utajiri wa Messi na Ronaldo

Forbes wametoa list ya wanamichezo 100 matajiri duniani, kwa upande wa TOP 10 mchezo wa soka ambao ndio unatazamiwa kuwa unaingiza hela nyingi, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi pekee ndio wamefanikiwa kuwa na utajiri uliowafaya waingie TOP 10. Ronaldo ndio ameongoza katika list ya wanamichezo matajiri duniani kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania, Lionel Messi ameshika nafasi ya pili kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 81.4 ambazo ni zaidi ya bilioni 178 za kitanzania. Cristiano Ronaldo utajiri wake wa dola milioni 32 ambazo ni zaidi ya bilioni 70 za kitanzania unatokana na mikataba ya matangaza kupitia account zake za social network kama twitter, instagram na facebook.

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 27.11.2017

Barcelona watarejea kumtafuta tena kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 25, soko litakapofunguliwa tena Januari. (Don Balon). Manchester City nao wanafikiria kuwasilisha ombi la kumtaka beki wa Real Sociedad wa miaka 26 kutoka Uhispania Inigo Martinez mwezi Januari. (Sun) Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku huenda akapigwa marufuku mechi tatu - ikiwa ni pamoja na debi ya Manchester - iwapo FA wataamua kumuadhibu mchezaji huyo wa miaka kwa 24 kwa kile kinachoonekana kuwa kama kumpiga teke beki wa Brighton Gaetan Bong. (Daily Mail) Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji amesifiwa sana na meneja wa Manchester United Jose Mourinho, licha ya kutofunga bao lolote katika mechi tisa kati ya 10 alizochezea klabu hiyo karibuni. (Guardian) Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema winga wa Wales Gareth Bale, 28, hatauzwa wakati wa dirisha ndogo la kuhama wachezaji Januari. (Daily Star) Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wanapanga kuwasilisha ofa ya £80m ku...

Huenda Lukaku akaikosa Manchester derby.

Mshambuliaji ghali wa Manchester United Romelu Lukaku huenda akafungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo endapo atakutwa na hatia baada ya kuonekana akimpiga teke beki wa timu ya Brighton, Gaetan Bong. Endapo Lukaku atakutwa na hatia huenda akafungiwa kutocheza mechi tatu. Moja kati ya mechi hizo ni ile ya watani wa jadi kati ya Manchester United na Manchester city.

Valencia 1 Barcelona 1. Messi anyimwa goli.

  Usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Valencia mambo yalikuwa magumu kwa FC Barcelona baada ya kulazimisha sare ya bao moja kwa moja. Pia mshambuliaji hatari wa FC Barcelona alifunga bao ambalo lilikataliwa na waamuzi wa mchezo huo. Bao la pekee lililo fungwa na FC Barcelona lilifungwa na beki wa timu hiyo      Jord Alba ambaye pia aliwahi kuichezea Valencia baada ya kupewa pasi kutoka kwa Lionel Messi.

Mkataba wa Messi wamtibua Ronaldo.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeripotiwa kuwa na "ghadhabu" juu ya mkataba wa mpya wa Lionel Messi na Barcelona Baada ya miezi ya tetesi tele, ilithibitika Jumamosi kuwa Mwargentina huyo alimwaga wino kusaini mkataba mpya utakaombakiza Camp Nou hadi 2021. Messi mwenye umri wa miaka 30 sasa imeripotiwa kuwa amesaini mkataba mnono wenye thamani ya €700m (£626m), na mshahara wake kuongezeka hadi £525,000 kwa juma - sawa na £90m katika kipindi chote cha mkataba wake. Kiasi hicho kinampa Messi ujira wa takribani 50% juu zaidi ya Ronaldo, ambaye inaaminika analipwa £360,000 kwa juma na Los Blancos. Kwa mujibu wa Diario Gol, Ronaldo "alilipuka kwa hasira" aliposikia habari za mkataba mpya wa Messi kwani ameshindwa kuimarisha mkataba wake binafsi kwa miezi mingi. Mshambuliaji huyo wa Kireno yupo kwenye mkataba hadi 2021 lakini imeripotiwa kuwa hana furaha na maisha ya jiji la Madrid na alikuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kurudi Manchester Unit...

PSG yaongoza mbio kumuwania Sanchez.

Paris Saint-Germain inaitangulia Manchester City katika mbio za kumfukuzia nyota wa Arsenal Alexis Sanchez Januari, The Mirror limeripoti. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile unafikia ukomo mwisho wa msimu huu, na PSG imeripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kumsajli kwa mkataba wa awali wanapojipanga kumruhusu Neymar kwenda Real Madrid msimu ujao wa majira ya joto.

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 26.11.2017

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo, 32, amefanya mazungumzo ya siri na PSG (DiarioGol, in Spanish) Alan Pardew anatarajiwa kuteuliwa kuwa mkufunzi mpya wa West Brom na inatarajiwa kwamba mkufunzi huyo wa zamani wa Crystal Palace huenda akaanza kazi siku ya Jumatatu.. (Sun) Kiungo wa kati wa Ujerumani na Arsenal Mesut Ozil, 29, atapewa mkataba wa dau la £350,000 kwa wiki ili kuhamia Barcelona (Daily Mirror) Lakini mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekana kwamba hakuna mazungumzo yoyote ya Ozil kuondoka katika klabu hiyo ya uwanja wa Emirates (Daily Star) Mkufunzi Antonio Conte anaitaka Chelsea kusuluhisha swala la kandarasi mpya ya kipa Thibaut Courtois. (Guardian) Vyombo vya habari vya Ubelgiji vinadai kwamba Courtois, 25, anataka kulipwa Yuro 230,000 kwa wiki (£205,000) ili kupata mshahara sawa na kipa David de Gea katika klabu ya Manchester United. (HLN, in Dutch) Mkufunzi wa zamani wa West Brom Tony Pulis anaongoza orodha ya wachezaji wanaotarajiw...

Wenger azitimulia vumbi Man Utd, Barca

Wenger yupo tayari kupambana na klabu za Barcelona na Manchester United kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. In the headlines Wenger azitimulia vumbi Man Utd, Barca SUNDAY NOVEMBER 26 2017 LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ameamua kuanzisha mbio za kumsaka nyota wa Monaco na timu ya taifa Ufaransa Thomas Lemar katika dirisha la usajili la Januari mwakani. Wenger yupo tayari kupambana na klabu za Barcelona na Manchester United kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. Mchezaji huyo kwa sasa ni habari ya mjini kutokana na kiwango chake anachokionyesha klabuni, na kinachovutia timu kubwa duniani ni kitendo chake cha kuipa ubingwa timu yake katika msimu uliopita. Katika dirisha la usajili lililopita, Wenger alijaribu kumnasa mchezaji huyo na hata alitoa ofa ya Pauni 90 milioni katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili kujaribu kuishawishi Monaco imwachie mchezaji huyo lakini ilishindikana. Lemar, ambaye alijiunga na Monaco mwak...

Simba 1 - 1

watoka sare 1-1 Kwa matokeo hayo, Simba anaendelea kuongoza ligi na pointi 23, akifuatiwa na Azam yenye 22 na Yanga ya tatu ina 21.

Bao la lala salama laipa Arsenal ushindi

26 Novemba 2017 Bao la lala salama laipa Arsenal ushindi Alexis Sanchez amefunga penalti katika muda wa kuyoyoma na kuipa Arsenal ushindi dhidi ya Burnley uwanjani Turf Moor. Ilikuwa ni marudio ya mechi ya msimu uliokwisha kati ya timu hizo mbili uwanjani Emirates wakati raia wa Chile - Sanchez alipofunga bao kunako dakika 98 kushinda mechi hiyo. Ilikuwa pia ni mara ya tatu mtawalia kuwa Gunners imepata ushindi katika muda wa mwisho wa mechi dhidi ya Clarets. Pointi tatu iliyojinyakulia Arsenal inaikweza timu hiyo hadi katika nafasi ya nne kwenye orodha wakati wakisubiria mechi yao dhidi ya wapinzani wao wa Londona kaskazini Tottenham, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya West Brom Jumamosi. Matokeo hayo yalikuwa ni kipigo kwa upande wa Sean Dyche ikiwa wamefanikiwa ushindi wa mechi zao mpaka sasa ikiwa walionekana kama watanyakuwa japo pointi moja, kabla ya refa Lee Mason kuashiria sehemu ambapo mlinzi James Tarkowski alimsukuma Aaron Ramsey. Petr Cech ndiyo aliyekuwa na kibarua kigu...