Tottenham ina matumaini ya kunasa saini mchezaji wa Paris St-Germain Lucas Moura kwa ada zaidi ya £ 20m. Mchezaji wa kimataifa wa Brazil, 25, amekutana na meneja wa Spurs Mauricio Pochettino na mwenyekiti Daniel Levy na anataka kukamilisha hatua hiyo. Lucas alijiunga na PSG kwa £ 33.5m kutoka Sao Paulo mwaka 2013 lakini ameonekana mara sita tu msimu huu na ameambiwa anaweza kupata klabu mpya. Ameshinda vikombe 13 vya ndani wakati akiwa nchini Ufaransa, ikiwa ni pamoja na vikombe vya ligi vinne.