Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mamelody Sundowns kumenyana na Barcelona Mei 16.

Uongozi wa klabu ya Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini umethibitisha rasmi kuwepo kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uhispania Barcelona. Mchezo huo utachezwa Mei 16 katika Uwanja wa FNB ikiowa ni sehemu ya maadhimisho ya kusherekea miaka 100 tangu kuzaliwa kwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Nelson Mandela. Hii itakuwa mara ya pili kwa klabu hizo kucheza nchini Afrika Kusini, mara ya kwanza ilikuwa 2007 ambapo Barcelona ilishinda mabao 2-1. Awali chama cha soka nchini Afrika Kusini, SAFA kilibariki uwepo wa mchezo huo baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumanne. Mbali na Mamelod, mchezo huo unaandaliwa pia kwa ushirikiano na Serikali ya Afrika Kusini, Mfuko wa Patrick Motsepe na Mfuko wa Nelson Mandela.
Machapisho ya hivi karibuni

Upepo wa La Liga

Zikiwa zimebaki mechi mbili msimu wa 2017/18 wa La Liga kumalizika, Real Madrid wana pointi 72 na endapo watashinda mechi zao zote wataishia kupata pointi 78 tu. Msimu wa mwisho Real Madrid kupata pointi chache zaidi kwenye La Liga, ulikuwa msimu wa 2008/09 - ambapo Los Blancos wakiwa chini ya Juande Ramos, hawakushinda taji lolote, wakiwaangalia Barcelona chini ya Pep Guardiola wakishinda mataji matatu na kuwafunga Madrid 6-2 nyumbani kwao Bernabeu. : Msimu huu mambo yanaweza kuwa tofauti, Madrid wapo kwenye fainali ya ulaya na endapo watashinda watakuwa wamefanikiwa kimataifa lakini watakuwa wamefeli nyumbani tena - mpaka hivi sasa wapo nyuma kwa pointi 18 nyuma ya Wakatalunya ambao tayari wameshabeba ubingwa. Leo usiku Madrid atakuwa akiumana na Celta Vigo

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Liverpool watinga fainali ligi ya mabingwa ulaya

Pamoja na kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa As Roma, lakini Liverpool wamefanikiwa kufudhu kwenda fainali ya michuano ya Champions League kwa aggregate ya mabao 6-7, na hii ikiwa ni fainali yao ya 8 wanakwenda. Roberto Firminho alitoa assist iliyozaa bao la kwanza la Liverpool lililofungwa na Sadio Mane, assist ya Firminho inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika miaka 10 ya mwisho ya CL kuwahi kuwa na walau mabao 7 na assist 7 katika msimu mmoja wa CL. Dakika ya 15 ya mchezo, As Roma walipata bao baada ya James Milner kujifunga. Hili linakuwa bao la kwanza kwa Liverpool kujifunga tangu Johne Arne Riise ajifunge katika mchezo wa nusu fainali vs Chelsea msimu wa 2007/2008. Dakika ya 25 Liverpool walipata tena bao la kuongoza kupitia kwa Gerginio Wijnaldum, na hili likiwa bao la 19 kwa Wijnaldum kuwahi kuzifungia timu za Uingereza, 11 akiwafungia Newcastle na 8 akiwafungia Liverpool. Bao la Mane limeufanya utatu wa Liverpool kufikisha jumla ya mabao 29 katika Champions League msimu huu...

INIESTA ATANGAZA RASMI KUONDOKA BARCELONA

Legend wa Barcelona Andres Iniesta ametangaza ataondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika Iniesta,33, amedumu Barcelona kwa miaka 22 huku akichukua vikombe 31 na timu hiyo. Ameichezea Barca mechi 669 tangu acheze mechi yake ya kwanza mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 18 Kiungo huyo ametangaza maamuzi hayo leo huku akibubujikwa na machozi mbele ya mkewe,watoto wake na wachezaji wenzake. Baada ya kuondoka hapo anataraji kujiunga na Chongqing Dangdai inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.

Kwa mara ya nne, Salah mchezaji bora ligi ya mabingwa ulaya msimu huu.

Mohammed Salah amechaguliwa mbele ya Marcelo wa Madrid kuwa mchezaji bora wa wiki ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya nne msimuu huu, magoli yake mawili yaliisaidia kuipa Liverpool ushindi wa goli 5-2 dhidi ya AS Roma nusu fainali ya kwanza Anfield.

Ozil arushiwa kipande cha mkate na kukila.

Kiungo mchezeshaji wa Arsenal Mesut Ozil alirushwa kipande cha mkate jana wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya kwanza EUROPA LEAGUE dhidi ya Atletico Madrid na kula kipande cha mkate huo na kuuweka pembeni. Tumeweza kuona wachezaji kama Dani Alves alivyorushiwa ndizi uwanjani na kuila, sasa tofauti ni kwamba Alves alifanyiwa kama kitendo cha ubaguzi, kwa upande wa mkate bado imeshindikana kutafsiri inamaanisha nini. Watu wengi wamekuwa wakipinga wachezaji kufanya vitendo kama hivyo kwani haijulikani chakula hicho kimewekewa nini hivyo kuweka hatarini maisha ya mchezaji. Arsenal watasafiri mpaka Spain Alhamisi ijayo kucheza mechi ya marudiano ndani ya uwanja wa Metropolitano huku Atletico wakiingia na faida ya goli la ugenini.