Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

INIESTA ATANGAZA RASMI KUONDOKA BARCELONA

Legend wa Barcelona Andres Iniesta ametangaza ataondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika Iniesta,33, amedumu Barcelona kwa miaka 22 huku akichukua vikombe 31 na timu hiyo. Ameichezea Barca mechi 669 tangu acheze mechi yake ya kwanza mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 18 Kiungo huyo ametangaza maamuzi hayo leo huku akibubujikwa na machozi mbele ya mkewe,watoto wake na wachezaji wenzake. Baada ya kuondoka hapo anataraji kujiunga na Chongqing Dangdai inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.

Kwa mara ya nne, Salah mchezaji bora ligi ya mabingwa ulaya msimu huu.

Mohammed Salah amechaguliwa mbele ya Marcelo wa Madrid kuwa mchezaji bora wa wiki ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya nne msimuu huu, magoli yake mawili yaliisaidia kuipa Liverpool ushindi wa goli 5-2 dhidi ya AS Roma nusu fainali ya kwanza Anfield.

Ozil arushiwa kipande cha mkate na kukila.

Kiungo mchezeshaji wa Arsenal Mesut Ozil alirushwa kipande cha mkate jana wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya kwanza EUROPA LEAGUE dhidi ya Atletico Madrid na kula kipande cha mkate huo na kuuweka pembeni. Tumeweza kuona wachezaji kama Dani Alves alivyorushiwa ndizi uwanjani na kuila, sasa tofauti ni kwamba Alves alifanyiwa kama kitendo cha ubaguzi, kwa upande wa mkate bado imeshindikana kutafsiri inamaanisha nini. Watu wengi wamekuwa wakipinga wachezaji kufanya vitendo kama hivyo kwani haijulikani chakula hicho kimewekewa nini hivyo kuweka hatarini maisha ya mchezaji. Arsenal watasafiri mpaka Spain Alhamisi ijayo kucheza mechi ya marudiano ndani ya uwanja wa Metropolitano huku Atletico wakiingia na faida ya goli la ugenini.

BESIKTAS YAGOMA KUMALIZIA MECHI

ISTANBUL, Besiktas wamegoma kumalizia dakika 33 zilizobaki za mechi yao ya nusu fainali ya pili ya kombe la ligi dhidi ya Fernabahce iliyoishia kwenye vurugu nzito. Vurugu hizo zilianza na kwa kocha mkuu wa Besiktas Senol Gunes kurushiwa kiti na kuumia kichwani baada ya fujo zilizotokea baina ya pande hizo mbili. Shirikisho la soka Uturuki limetoa tamko kwamba mechi hiyo itaendelea ilipoishia Mei 3 bila mashabiki, Besiktas nayo imetoa taarifa ikisema kwamba hawatotokea siku ya mechi wakisisitiza ni wazi wao ndio walikuwa wahanga wa fujo zilizojitokeza. Mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya timu hizo iliisha kwa sare ya 2-2. Kwenye nusu fainali nyingine Akhisar Belediyespor imeingia fainali baada ya kuwatembezeshea bakora Galatasaray hivyo wanasubiri mshindi kati ya Besiktas na Fernabahce.

Orodha ya wafungaji ligi kuu Tanzania bara.

Huu ndiyo msimamo wa wafungaji wa ligi kuu soka Tanzania Bara mpaka sasa ikiwa klabu zimebakiza michezo michache klaba ya kujua nani atakae twaa tuzo ya mfungaji bora.

Barcelona yaweka rekodi mpya ligi kuu Hispania.

Klabu ya Barcelona jana usiku imeweka rekodi mpya nchini Hispania baada ya kuchomoza na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa Ligi kuu nchini humo La Liga. Barcelona inakuwa klabu ya kwanza kucheza michezo mingi (39) bila kupoteza kwenye La Liga na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na klabu ya Real Sociedad ya kucheza michezo 38 bila kupoteza rekodi ambayo iliwekwa msimu wa 1979/80. Kwa sasa Barcelona wanaongoza ligi kwa alama 82 mbele ya Atletico Madrid wenye alama 68 na Valencia wapo nafasi ya tatu na alama 65.

Arsenal na rekodi mbovu ugenini.

Pierre-Emerick Aubameyang anaweza kuwa mchezaji wa kwanza wa Araenal kufunga mabao katika mechi 5 mfululizo za Arsenal tangu Olivier Giroud afanye hivyo wakati yupo Arsenal mwaka 2015. Tayari Arsenal wamepoteza michezo 4 mfululizo ugenini,mara ya mwisho wanapoteza mechi 5 mfululizo ugenini ilikuwa 1984/1985 na mwaka huo baada ya mechi hizo walizopoteza ugenini walipata ushindi wa kwanza katika uwanja ambao leo ndio wanakwenda wa St James Park. Na kama hujui tu ni kwamba Arsenal hawajawahi kupoteza michezo 5 mfululizo ya ugenini katika calender ya mwaka mmoja tangu wafanye hivyo mwaka 1925, na kama leo watakubali kufungwa itakuwa mara yao ya kwanza ndani ya miaka 93. Lakini Newcastle wenyewe wanaonekana nj wanyonge sana kwa Arsenal, katika michezo 10 iliyopita ya Newcastle mbele ya Arsenal wamekubali kupoteza michezo yotee mbele ya washika mtutu hao wa London. Bao la Nolberto Solano mwaka 2005 ambalo liipa ushindi Newcastle mbele ya Arsenal, ndio ushindi wa mwisho kwa Newcastle ...

Andrés Iniesta kutimkia China.

Kiungo mkongwe wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Andrés Iniesta ameripotiwa kufikia makubaliano na klabu ya Tianjin Quanjian kutoka China kuanzia msimu ujao. Iniesta anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamfanya alipwe kiasi cha €37m sawa na zaidi ya bilioni 103 kila mwaka baada ya kodi.

Real Madrid vs Bayern Munich, Liverpool vs As Roma, kuna nn nyuma ya pazia!?

Ukurasa wa Twitter wa As Roma umeandika hivi “tutakuwa wapinzani kwa dakika 180, lakini lolote litakalotokea tutaendelea kuwa marafiki milele” huo ni ujumbe kutoka kwq As Roma kwenda kwa Mo Salah. Roma wameamua kumtumia Salah ujumbe huo baada ya ratiba ya nusu fainali ya Champions League kutoka na As Roma kujikuta mikononi mwa Liverpool ambayo ndio timu anayochezea Mo Salah kwa sasa. Liverpool wana rekodi nzuri sana mbele ya As Roma, wamepoteza mechi moja tu kati ya tano dhidi yao, wakisuluhu mbili na kushinda mbili ikiwemo fainali ya European Cup 1983/1984 ambapo Liverpool walishinda kwa matuta. Bayern Munich nao wameangukia tena kwa Real Madrid, hili ni bundi ambalo Bavarians hawataki kusikia. Katika michezo mitano ya mwisho ambayo Real Madrid wamekutana na Bayern Munich wameshinda yote. Ukiacha rekodi ya Cristiano Ronaldo ya mabao 9 katika mechi 6 dhidi ya Bayern Munich lakini gwiji wa zamani wa Bayern Munich Roy Makaay anashikilia rekodi ya goli la haraka zaidi UCL(s...

Lionel Messi anapofunga mji wa Barcelona hutetemeka.

Wakati Lionel Messi anapofunga mji wa Barcelona hutetemeka. Wanasayansi waliweka vifaa vya kupima tetemeko la ardhi katika uwanja wa Camp Nou na kufanikiwa kupima mitetemeko ya ardhi kila nyota huyo wa Barcelona anapofunga. Athari ya mabao yake huonekana katika data kila wakati mashabiki wanaposheherekea kwa kuruka juu na chini uwanjani. Vipimo hivyo vilidhihirika wakati Barcelona ilipofanya miujiza ya kutoka nyuma na kuishinda klabu ya Paris Saint Germain katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu uliopita. Huku wakiwa 4-0 katika awamu ya kwanza ya makundi ya muondoano ,timu hiyo ilifunga bao la dakika za lala salama na kupata ushindi wa jumla ya 6-5 nyumbani. Miujiza ya Messi anapofunga katika kipimo Tetemeko la ardhi linalosababishwa na kandanda limejadiliwa katika kongamano la sayansi la Ulaya mji wa Vienna Austria. Ni kazi ya Jordi Diaz na wenzake katika taasisi ya sayansi ya  iliopo katika mji mkuu wa Catalonia. Kile ambacho Diaz amegundua ni tofauti iliopo kati ya mas...

Ronaldo aweka rekodi UEFA, Sevilla kibarua kigumu dhidi ya Bayern.

Ni Cristiano Ronaldo tena anaendelea kuwanyamazisha wapinzani waReal Madrid, dakika ya 3 tu alipigashuti lake la 9 kwa Gianluigi Buffoon na kufunga baolake la 8 dhidi ya golikipa huyo, hili likiwa baola kwanza katika mchezo huu. Dakika ya 64 Cristiano Ronaldo tena aliifungia Real Madrid bao la pili na kumfanya kuwa mchezaji katika historia aliyewafunga Juve mabao mengi (9) kabla yaMarcelo kufungia baola 3 Real Madrid. Hii ni mara ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009 walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu. Kama hujui tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio baola mapema zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa namabao 38 katikamsimuhuu (michuano yote)ikiwaniidadi kubwa kuliko mchezaji yeyote barani Ulaya. Tangu klabu ya Juventus wahamie katika uwanja wao mpya mwaka 2011 hawajawahi kupokea kipigo kama hiki katika ...