Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeripotiwa kuwa na "ghadhabu" juu ya mkataba wa mpya wa Lionel Messi na Barcelona
Baada ya miezi ya tetesi tele, ilithibitika Jumamosi kuwa Mwargentina huyo alimwaga wino kusaini mkataba mpya utakaombakiza Camp Nou hadi 2021.
Messi mwenye umri wa miaka 30 sasa imeripotiwa kuwa amesaini mkataba mnono wenye thamani ya €700m (£626m), na mshahara wake kuongezeka hadi £525,000 kwa juma - sawa na £90m katika kipindi chote cha mkataba wake.
Kiasi hicho kinampa Messi ujira wa takribani 50% juu zaidi ya Ronaldo, ambaye inaaminika analipwa £360,000 kwa juma na Los Blancos.
Kwa mujibu wa Diario Gol, Ronaldo "alilipuka kwa hasira" aliposikia habari za mkataba mpya wa Messi kwani ameshindwa kuimarisha mkataba wake binafsi kwa miezi mingi.
Mshambuliaji huyo wa Kireno yupo kwenye mkataba hadi 2021 lakini imeripotiwa kuwa hana furaha na maisha ya jiji la Madrid na alikuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kurudi Manchester United majira ya joto.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni