Miamba ya soka kutoka London, Chelsea wako mbioni kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang ambaye anaonekana kutokuwa na moyo wa kuichezea klabu hiyo tena.
Klabu ya Borussia Dortmund imeziarifu baadhi ya timu kuwa atakuwa sokoni Januari mwakani.
Klabu za Arsenal na Liverpool ziko katika upinzani wa kumnyakua winga wa PSG Julian Drexler. Liverpool wamekuwa wakimuhitaji winga huyo kwa mkopo lakini PSG wamesisitiza kuwa anauza. Pia ikumbukwe kabla ya Draxler kwenda PSG alikuwa akihitajika na washika bunduki wa London.
Pia klabu ya FC Barcelona bado wanajiandaa kumnasa kiungo wa klabu ya Tottenham katika dirisha dogo la usajili. Miamba hiyo inaami kuwa anaweza kuwa mbadala wa Andres Iniesta ambaye soka lake linaelekea ukingoni.
PSG wako mbele Manchester City katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez ambaye ana kila dalili za kuondoka klabuni hapo Januari mwakani. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Chile unafikia ukomo mwakani Januari.
Klabu ya Borussia Dortmund, inataka kumsajili mchezaji wake wa zamani Mikhitaryan anayekipiga huko Manchester United. Manchester United walimsajili mchezaji huyo kutoka Borussia Dortmund kwa dau la €30 milioni na sasa wako tayari kumsajili tena.
Ronaldo yuko tayari kwa mazungumzo na klabu ya PSG. Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake George Mendes afanye mazungumzo na viongozi wa klabu ya Paris Ufaransa. Mchezaji huyo wa Ureno anafanya hivyo ili kulazimisha mshahara mkubwa na anaamini PSG ndiyo wanaoweza kumtimizia mahitaji yake ya kifedha. Hii imekuja baada ya hasimu wake Lionel Messi kuongezewa mkataba mnono hadi mwaka 2021.
Kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeon anataka kumsajili kiungo wa PSG Javier Pastore, Pastore hana furaha na maisha ya klabuni PSG.
Maoni
Chapisha Maoni