Wenger yupo tayari kupambana na klabu za Barcelona na Manchester United kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.
In the headlines Wenger azitimulia vumbi Man Utd, Barca
SUNDAY NOVEMBER 26 2017
LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ameamua kuanzisha mbio za kumsaka nyota wa Monaco na timu ya taifa Ufaransa Thomas Lemar katika dirisha la usajili la Januari mwakani.
Wenger yupo tayari kupambana na klabu za Barcelona na Manchester United kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.
Mchezaji huyo kwa sasa ni habari ya mjini kutokana na kiwango chake anachokionyesha klabuni, na kinachovutia timu kubwa duniani ni kitendo chake cha kuipa ubingwa timu yake katika msimu uliopita.
Katika dirisha la usajili lililopita, Wenger alijaribu kumnasa mchezaji huyo na hata alitoa ofa ya Pauni 90 milioni katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili kujaribu kuishawishi Monaco imwachie mchezaji huyo lakini ilishindikana. Lemar, ambaye alijiunga na Monaco mwaka 2015 akitokea Caen amekuwa akichezea kikosi cha kwanza cha Ufaransa kwa muda sasa na kocha Wenger anaamini ndio suluhisho pekee kwa kikosi chake baada ya kuondoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil, ambao wana kila dalili ya kuondoka klabuni hapo Januari mwakani.
Maoni
Chapisha Maoni