Yanga imechoshwa na visa na vituko vya mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma na sasa inapanga namna ya kumwajibisha
Klabu Yanga imepanga kumuwajibisha mshambuliaji wake raia wa Zambabwe Donald Ngoma, kwa kosa la kwenda kwao bila ruhusu ya klabu hiyo ambayo anaitumikia kwa msimu wa tatu sasa.
Chanzo cha bari kutoka ndani ya klabu hiyo kimeiambia Goal , kuwa uongozi wa juu upo katika mjadala wakijadili namna ya kumwadhibu mchezaji huyo ambaye hajaichezea timu yao kwa miezi miwili baada ya kutimkia kwao Zimbabwe bila ruhusa ya klabu.
"Tupo kwenye kikao cha kumjadili Ngoma, amekuja jana kutoka kwao Zimbabwe tunachotaka ni kutuambia nani alimpa ruhusa ya kwenda kwao na kingine tunataka kujua kama anataka kucheza Yanga au kuondoka maana tunashindwa kumuelewa kwa yale anayotufanyia," imesema taarifa hiyo.
Chanzo hicho kimedai pamoja na majeruhi aliyokuwa nayo mchezaji huyo lakini alipaswa kubaki nchini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu kama ilivyo kwa wenzake wawili Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko, lakini yeye aliamua kuondoka kwa maamuzi yake kana kwamba siyo mwajiriwa wa Yanga.
Tangu msimu uliopita Ngoma, amekuwa akiisumbua Yanga na mchango wake kwenye timu umekuwa mdogo ukilinganisha na ilivyokuwa msimu wake wa kwanza ambapo aliweza kufunga mabao 24, katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo na kuifikisha hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni