Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Dembele kuikosa El classico

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa Ousmane Dembele hatacheza mechi ya Clasico wikiendi ijayo licha ya kuanza mazoezi
Dembele hajacheza tangu alipopata majeraha dhidi ya Getafe Septemba, na kulazimika kukaa nje kwa miezi. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa Kifaransa amerejea kwenye ratiba ya mazoezi, na kuamsha tetesi kuwa anaweza kuwemo kwenye safari ya kwenda Real Madrid Desemba 23.

Lakini Valverde amesema Dembele hatarejea kibaruani hadi Januari, akisisitza kuwa hakuna haja ya kumuingiza mchezaji huyo matatizoni.
"Amefanya mengi kwenye mazoezi wiki hii, lakini hajakamilisha mazoezi kamili hadi sasa," kocha aliwaambia waandishi Jumamosi.

"Wiki ijayo tutamwongezea kazi, lakini mpango ni ule ule wa awali. Januari ndio tunamtarajia kurudi dimbani.
"Itakuwa mapema - na tutamweka matatizoni kumchezesha mapema. Malengo yetu ni kumwacha kwanza hadi Januari."

Kabla ya safari kwenda Bernabeu kwa mechi ya kwanza ya Clasico kwa msimu huu, wataikaribisha Deportivo La Coruna kwenye uwanja wa Camp Nou, na Andres Iniesta na Javier Mascherano watarudi mchezoni Jumapili.

Nahodha Iniesta alikosa mechi mbili za mwisho za Barca kwa sababu ya tatizo la misuli lakini amepona na yupo tayari kwa mechi ya wikiendi hii, wakati Mascherano hajacheza tangu katikati ya mwezi Novemba alipopata majeraha kwenye majukumu ya ktaifa Argentin

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...