Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hazard atamani kutua Madrid

Mazungumzo baina ya Chelsea na Eden Hazard kwa ajili ya mkataba mpya yamesimama kwani Mbelgiji huyo anataka kutimkia Real Madrid kwa mujibu wa The Times .
Imeripotiwa kuwa Blues wapo tayari kumfanya Hazard kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, kwa mshahara wa £300,000 kwa wiki.

Lakini Hazard anasita kuongeza mkataba na bado amebakiwa na miaka miwili na nusu kwani anahofu kukosa kutimiza ndoto ya kujiunga na Los Blancos.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez anafikiria kumtoa Toni Kroos kwa Juventus ili ampate Paulo Dybala kama biashara ya kubadilishana, kwa mujibu wa Rai Sport .

Thibaut Courtois ataruhusiwa kuondoka kama mchezaji huru Chelsea ifikapo 2019 kwani Mbelgiji huyo ameendeea kukataa kusaini mkataba mpya kwa mujibu wa, The Sun .
Ikiwa Blues watashindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na mlinda mlango huyo - ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Real Madrid - atalazimika kumaliza mkataba wake badala ya kumuuza kabla ya kuumaliza mkataba.

Manchester United wataachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale kama Real Madrid hawataipunguza hadi nusu bei ya Gareth Bale, kwa mujibu wa The Mirror .
Los Blancos wanaamini thamani ya Bale ni £100 milioni, lakini Mashetani Wekundu wanataka saini yake kwa £50-60m.

Imeripotiwa kuwa Juventus wanamfuatilia kinda wa Kibrazili anayekipiga Sao Paulo, Eder Militao wakiwa na lengo la kumleta Turin, kimedai calciomercato.com .
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akicheza mechi nyingi kwenye klabu ya Dorival Junior, kama beki mpya. Militao pia anaweza kucheza kama beki wa kati na kiungo.

Crystal Palace ambao wapo kwenye hatari ya kushuka daraja Ligi Kuu Uingereza wamegeuzia macho yao kwa mlinda mlango wa Paris-Saint Germain Kevin Trapp, kwa mujibu wa Sun .

Manchester City wanajipanga kumfanya Raheem Sterling kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye Ligi ya Uingereza kwa kumlipa £300,000 kwa wiki, kwa mujibu wa The Sun .

Neymar amefikia makubaliano na rais wa Real madrid Florentino Perez ambayo yatamwezesha kujiunga na miamba hiyo ya Hispania 2019, kwa mujibu wa Don Balon .

Alex Sandro ameendelea kuwaachia mlango wazi Chelsea kwani anafikiria kuondoka Juventus baada ya Kombe la Dunia 2018, kimedai TMW .
Beki huyo mahiri amekuwa akihusishwa sana na tetesi za kujiunga na Blues dirisha la majira ya joto na kiwango chake Kombe la Dunia akiwa na Brazili ndicho kitakachoweza kumsaidia kutua London.

Bosi wa Manchester United Jose Mourinho anamtaka Mesut Ozil kwenye kikosi chake ili kutatua matatizo ya nafasi ya namba 10, kwa mujibu wa
Telegraph .
Nyota huyo wa Arsenal atakuwa amemaliza mkataba wake majira ya joto na anasita kusaini mkataba mwingine, jambo linalowafanya wengi wahofu kwamba ataondoka.

Barcelona watampa Philippe Coutinho mkataba wenye thamani ya €14 milioni kwa msimu ikiwa watafanikiwa kuishawishi Liverpool kumuuza Mbrazili huyo, kimedai Sport .
Liverpool walikataa ofa zote kwa ajili ya Coutinho majira ya joto, lakini Barca wanataka kurudi upya Januari na wapo tayari kutoa ofa ya €150m kwa ajili ya kiungo huyo.
Lakini kusajiliwa kwa Coutinho kuuza wachezaji watatu ili kuweza kumudu bajeti yao.

Wakuu wa Barcelona wameungana kuhakikisha Philippe Coutinho anasaini mkataba kujiunga na klabu hiyo Januari, kwa mujibu wa Sport .
Mesut Ozil amependekezwa kuwa mbadala Barce ikiwa miamba hao wa Catalan watashindwa kuishawishi Liverpool kumuuza Coutinho dirisha dogo la uhamisho.
Lakini habari zimedai kuwa Coutinho bado anataka kuondoka Anfield, na kwamba ofa itakayofikia €150 milioni itatosha kuishawishi Liverpool kumuuza, na Liverpool haitaki kufikiria mchezaji mwingine tofauti.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...