England. Liverpool watakuwa nyumbani huko Anfield leo kuwakaribisha Everton mechi itakayopigwa saa kumi na moja na robo (11:15 jioni).
Timu hizo zinakwenda kwenye mechi hiyo kila moja ikiwa katika hali nzuri baada ya kushinda mechi zao zilizopita, ambapo Everton ilishinda mabao matatu ugenini kwenye Europa League, huku Liverpool ikimpiga mtu mabao saba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mechi nyingine ya leo, Arsenal iliyoshinda BATE 6-0 watakuwa na shughuli pevu ugenini kwa Southampton.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni