Wawili hao wataendeleza uhasimu wao katika Old Trafford Jumapili mchana City watakapoikabili Manchester United katika mechi ya vinara wa ligi
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa yeye na Jose Mourinho ni 'kama mapacha' kutokan na shauku zao kutwaa mataji.
Wawili hao wataendeleza uhasimu wao katika Old Trafford Jumapili mchana City watakapoikabili Manchester United katika mechi ya vinara wa ligi.
Guardiola na Mourinho hawajawahi kutazamana machoni, mara ya kwanza wakianza wakiwa Hispania Barcelona na Real Madrid, lakini kocha huyo wa City amesema wanafanana kuliko watu wanavyodhani.
Alipoulizwa kama Mourinho naye amedhamiria kutwaa mataji, Guardiola aliwaambia waandishi: "Kabisa! Katika hilo sisi ni mapacha. Anataka kushinda mataji, Nataka kushinda mataji.
"Antonio Conte kama ilivyo kwa Jurgen Klopp na Mauricio [Pochettino]. Tunapenda kushindana, tunapenda kushinda mechi lakini amini maneno yangu, wala si jambo la kipekee kwetu kuzifunga timu za Mourinho.Tumekutana mara nyingi katika nyakati kubwa."
Guardiola anamzidi Mourinho kwa kushinda mechi nane katika mechi 19.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni