Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sanchez anauzwa 35 million tu.

HAYA! Alexis Sanchez huyo hapo, mchukueni! Arsenal imesema hivi, staa huyo wa Chile atakuwa huru tu kwenda kwenye timu yoyote anayotaka kama tu itawekwa Pauni 35 milioni mezani.
Kwa lugha nyepesi tu. Arsenal inampiga bei staa wake huyo kwa Pauni 35 milioni. Ndiyo, Pauni Thelathini na Tano milioni tu.

Sanchez aligomewa kwenda Manchester City kwenye dirisha lililopita na kocha Arsene Wenger alidai kwamba hamuuzi kwenye dirisha la Januari, lakini kwa sasa anaonekana kuanza kulegeza masharti.
Kwa sababu mkataba wa mchezaji huyo utafika tamati mwisho wa msimu na kwamba ataondoka bure, Arsenal kwa sasa wamemua ni heri wakaambulia chochote kuliko kumshuhudia mchezaji huyo mahiri kabisa kuondoka bila ya kupata chochote.

Kutangazwa kwa dau hilo kuna maana kwamba sasa Manchester City, Paris Saint-Germain, Bayern Munich na timu nyingine zinazohitaji huduma yake ni wakati wao tu kuanza kupeleka ofa zao kwa ajili ya kupata huduma yake.
Mchezaji mwenyewe anataka kuachana na Arsenal kwa haraka iwezekanavyo na anachoombea ni Man City wapeleke hizo Pauni 35 milioni.

Arsenal imeripotiwa kutangaza bei hiyo kwa sababu tu inataka mteja wa haraka Januari huku wakipanga kumharibia staa huyo baada ya kudaiwa kwamba, amepanga kujiunga na Man City mwishoni wa msimu ili akapewe mkataba wenye thamani ya Pauni 400,000 kwa wiki.
Uamuzi huo ina maana timu yoyote itakayoleta mkwanja ambao, Arsenal inataka kwenye dirisha la Januari, basi Sanchez anapigwa bei.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...