Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 29 December 2017

Njia itakuwa nyeupe kwa Barcelona kumsajili Antoine Griezmann kwa kitita cha paundi £89 milioni kwani Manchester United hawatafanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid kwa mujibu wa Marca .

Barcelona bado inataka kumsajili Angel Di Maria, na Paris Saint-Germain imetaja bei yake kuwa £45 milioni kwa mujibu wa ESPN .Mwargentina huyo si mchezaji muhimu sana kwa PSG tangu ujio wa Neymar na Kylian Mbappe.

Tottenham wamedhamiria kusambaratisha bajeti yao ili kuweza kumbakisha Harry Kane kwenye klabu yao, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa kinara wa mabao 2017 akifunga magoli 56, kwa sasa analipwa £110,000 kwa wiki kiasi ambacho ni kidogo kwa wachezaji wa kaliba yake.
Mshahara wa Kane utakuwa unaongezeka kwa mara ya nne tangu Agosti 2014, Spurs wakilenga kuzipindua ofa za Real Madrid.

Klabu za Uingereza zimepata fununu kuwa huenda meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anaweza kumruhusu kuondoka winga wake Yannick Carrasco, kwa mujibu wa AS .
Manchester United na Chelsea zimetajwa kwenye tetesi za kutaka kumsajili Mbelgiji huyo miezi ya hivi karibuni, Mkataba wa Carrasco una thamani ya £86 milioni.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...