Manchester United wanafuatilia kwa karibu ripoti za tofauti baina ya Cristiano Ronaldo na viongozi wa Real Madrid, kimedai Mirror .
Magazeti yanasema kuwa uhusiano baina ya Ronaldo na Florentino Perez umevunjika, jambo linaloleta shaka juu ya mustakabali wake Bernabeu
Philippe Coutinho anaelekea kuwa mchezaji ghali zaidi kuuzwa Ligi Kuu Uingereza katika historia akitarajiwa kutua Barcelona kwa kitita cha £125 milioni, kwa mujibu wa Express .
Mbrazili huyo alikuwa shabaha ya Barca miezi mingi, lakini Blaugrana walishindwa kufikia makubaliano na Liverpool majira ya joto.
Nyota wa Inter Joao Mario ameingia kwenye arada za Manchester United wakitaka kumsajili kuziba pengo la Henrikh Mkhitaryan, kwa mujibu wa Sun .
Hali si shwari kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Armenia katika Old Trafford, na klabu nyingi zinaitaka saini yake.
Ikiwa atatimkia Serie A, United watafanya jaribio la kumsajili Mreno wa Nerazzurri kwa kiasi cha paundi milioni 40.
Real Madrid wanafikiria kumsajili beki mahiri wa Barcelona, Samuel Umtiti, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez anataka kusajili beki mpya wa kati, lakini ameanza kupata hofu ya kutoa hela ndefu baada ya Liverpool kutoa £75 milioni kwa ajili ya Virgil van Dijk.
Maoni
Chapisha Maoni