Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya

Manchester United itafanya mchakato kumsajili kiungo wa Real Madrid Marco Asensio dirisha la uhamisho la Januari baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale, kwa mujibu wa Don Balon .
Mashetani Wekundu wanajiamini watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo wa miaka 21 kwani ameshindwa kupata nafasi ya kudumu Santiago Bernabeu.

Manchester United wapo tayari kusikiliza ofa kuwauza mabeki wao Luke Shaw na Matteo Darmian, kwa mujibu wa The Daily Record .
Shaw ambaye amesumbuliwa na majeraha amepewa nafasi kujiunga na klabu nyingi za Uingereza wakati Muitaliano Darmian hatakiwi kwenye kikosi cha Jose Mourinho.
United wanataka kutunisha mfuko wao ili kuwasajili beki wa kushoto Alex Sandro na Danny Rose majira ya baridi.

Real Betis wanaandaa ofa kumsajili Daniel Sturridge kutoka Liverpool, kwa mujibu wa El Gol Digital .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akihaha kutafuta muda wa kucheza zaidi Anfield na atapewa nafasi kutimkia Hispania Januari.

Chelsea wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 20 kwa ajili ya winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, limedai The Sun .
Blues wamekuwa wakimfuatilia Mjamaica huyo kwa kipindi cha miezi 18 na wanataka kuipiku Barcelona kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20.
Jose Mourinho amemfanya Alex Sandro wa Juventus kuwa shabaha nambari moja kutua Manchester United kucheza nafasi ya beki wa kushoto kwa mujibu wa Daily Record .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...