Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wenger: Manchester united hawajaonyesha nia ya kumtaka Ozil

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa Manchester United hawajawasiliana na Gunners kuhusu uhamisho wa Mesut Ozil.

Kiungo huyo akiwa amebakiwana miezi sita tu kwenye mkataba wake, klabu kadhaa ikiwa ni pamoja na United zimehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Mjerumani huyo.

Hata hivyo, akidai kuwa hana uhakika kuhusu maendeleo ya mazungumzo na Ozil, Wenger amesisitiza kuwa kiungo huyo hataondoka London Kaskazini kabla ya mwisho wa msimu.

Mfaransa huyo aliwaambia waandishi: "Karibu kiasi gani? Sijui ni karibu kiasi gani. Man United hawajawahi kutupigia, kwa hiyo sijui jambo hilo limekujaje.

"Hilo ni jambo ambalo limezushwa. [Atabaki] hadi mwisho wa msimu, mengine yapo wazi."

Pamoja na kuwa Ozil amefunga magoli mawili na sare tano katika mechi 14 Ligi Kuu Uingereza msimu huu, hajafanikiwa kufunga katika mechi tatu za mwisho.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...