Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema pamoja na malumbano yote na mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma lakini haitavunja mkataba naye.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara Hussein Nyika, amesema matatizo yaliyotokea Kati Yao na Ngoma ni ya kawaida ambayo wanaweza kukaa mezani na kuyamaliZa hivyo hawana mpango wa kuachana na mchezaji huo.
"Maneno yamekuwa mengi kwenye vyombo vya Habari kuhusu kupishana kwetu na Ngoma kitu cha msingi hapa ambacho naweza kuwaeleza wale watu wanaotaka tuachane na Ngoma hilo halitotokea tutakaa chini chini kuyazungumza na hatimaye kuyamaliza," amesema Nyika.
Kiongozi huyo amesema anajua kwamba wanao paisha jambo hilo ni wapinzani wao Simba ambao lengo lao ni kumchukua mchezaji huyo na hilo halitowezakana kutokana na kushtukia mpango wao.
Ngoma alingia kwenye mgogoro n uongozi was timu yake baada ya kujiamlia kwenda kwao Zimbabwe kujiuguza bila ruhusa kutoka kwa viongozi wa timi na uongozi was timu umepanga kumwakilisha ili kutoa mfano kwa wachezaji wengine wenye mawazo Kama hayo.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni