Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Alexis Sanchez kugharimu Manchester United

Ulidhani ni rahisi au ni bure kwa Alexis Sanchez kwenda Manchester United? Usijidanganye siyo bure hata kidogo, bali Manchester United watachomoka kiasi kikubwa sana cha pesa kwa mshambuliaji huyo.

£180m United wataitumia katika dili la Sanchez na katika pesa hiyo kiasi cha £35m kinatajwa kama kiasi ambacho Arsenal watavuna endapo watakubali kumuuza Alexis Sanchez kwenda Manchester United.

Kuna pesa nyingine ndefu sana ambayo ni £117m, kiasi hicho cha pesa United watatumia kumlipa mshahara Sanchez wakati wote atakapokuwa katika klabu hiyo na inatajwa kwamba mkataba wake atasaini miaka minne na nusu.

Halafu kuna £20m hii inatajwa ni pesa ambayo Sanchez anaweza kuipata toka United kama akimwaga wino kuitumikia klabu hiyo na usisahau kwamba wakala wake naye atapewa kiasi cha £10m.

Inatajwa kwamba United hawajali hata kidogo kuhusu pesa na wako tayari kutumia pesa yote hiyo kwa Alexis Sanchez ilimradi tu Sanchez asaini katika timu yao, usajili wa Sanchez unaonekana kukwama kwama na bado hakuna taarifa ya uhakika lini atasaini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...