Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte amefutilia mbali madai kuwa ana mpango wa kumsajili beki wa Juventus Giorgio Chiellini
Conte yupo sokoni kwa ajili ya kutafuta wachezaji wachache katika dirisha la uhamisho wa Januari na David Luiz amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa mbioni kuondoka Stamford Bridge, Chiellini akitajwa kuwa miongoni mwa wanaweza kuirithi nafasi yake.
Hata hivyo, licha ya kuwahi kufanya kazi na Muitaliano huyo hapo awali, Conte anasema kuwa hajafikiria kumleta Chiellini Premier League.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 sasa aliwaambia waandishi: "Kwenye soko la uhamisho kuna tetesi. Sisi tutafanya kilicho chema kwa ajili ya timu.
"Ni lazima niwe mkweli. Giorgio ni mchezaji shupavu na bora lakini anataka kumalizia soka lake Juventus. Ni sahihi kumaliza soka kwa namna hii."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amedumu Turin kwa muda wa miaka 12 na nusu, akicheza jumla ya mechi 453 katika michuano yote.
Maoni
Chapisha Maoni