Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Conte na Mourinho katika bifu la kupanga matokeo

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameendeleza vita ya meneno dhidi ya bosi wa Chelse Antonio Conte, akikumbushia adhabu ya Muitaliano huyo 2012 kwa kupanga matokeo.
Mameneja hao wawili wameingia kwenye mgogoro siku mbili zilizopita Conte akisema kuwa Mourinho ana tabia ya "utovu wa nidhamu pembezoni mwa chaki".

Msemo huo wa Conte aliutoa akimjibu Mourinho aliyebwata kuwa baadhi ya mameneja wa Premier League wana tabia "kama kijana chizi" wakati wa mechi - kauli ambayo ilimlenga bosi wa Chelsea.
Muitaliano huyo alidai kuwa Mourinho alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa mbaya wa kupoteza kumbukumbu, akitaja kwa msamiati wa Kiitaliano akimlenga bosi wa Man United.

"Nadhani anahitaji kujichunguza alivyokuwa huko hapo awali - labda alikuwa akijizungumzia alivyokuwa siku za nyuma," alisema Conte. "Labda, wakati mwingine, nadhani anasahau alichowahi kusema zamani, jambo ambalo ni tabia yake.

"Wakati mwingine nadhani analo tatizo, silijui jina, lakini demenza senile... pale unaposahau kile ulichokifanya wakati uliopita.
Baada ya Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Derby County kwenye mechi za Kombe la FA Ijumaa, Mourinho alifufua upya uhasama wao.
"Jambo pekee ninalotaka kusema kumaliza habari ni ndiyo, niliwahi kufanya makosa siku za nyuma kwenye mstari wa chaki," alisema Mourinho.

"Naam, nitapunguza, lakini nadhani bado nitaokesea kidogo. Jambo ambalo halijawahi kunitokea na kamwe halitatoke ni kufungiwa kwa kupanga matokeo.
"Hilo halijatokea kwangu na kamwe haitatokea."

Kauli za Mourinho zinarejea adhabu ya kufungiwa mechi nne aliyopewa Conte msimu wa 2012-13 akiwa meneja wa Juventus kwa kushindwa kutoa maelezo ya kupanga matokeo akiwa akiiongoza Siena.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...