David de Gea amejitangaza mwenyewe kuwa "mwenye furaha sana" huko Manchester United huku kukiwa na fununu zinazoendelea kuhusu suala la yeye kujiunga na vigogo wa La Liga Real Madrid.
"Unapofikiri niko msimu wangu wa saba sasa, mimi nina furaha sana japo kuna jambo moja au mawili ambayo hayajakaa sawa lakini bado ninafuraha sana. Nilikuja hapa kama mtoto lakini sasa ni mwanaume ndani na nje ya ya uwanja. Nikitazama nyuma ni miaka mizuri ajabu" alisema Mhispania huyo.
Maoni
Chapisha Maoni