Mchezo huo wa Premier League ulipigwa nyumbani kwa Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park ambapo licha ya kuongozwa na Wayne Rooney bado timu hiyo ilishindwa kufurukuta.
Mabao ya Man United katika mchezo huo yalifungwa na Anthony Martial katika dakika ya 57 na Jesse Lingard katika dakika ya 81.
Kutokana na matokeo hayo Man United imerejea nafasi ya pili kutoka ya tatu kwa kuwa na pointi 47 huku Chelsea ikifuatia kwa kuwa na pointi 45 licha ya kuwa yenyewe ipo nyuma mchezo mmoja na inatarajiwa kucheza na Arsenal, kesho Jumatano.
Maoni
Chapisha Maoni