Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Guardiola: Sanchez atabaki Arsenal.

Pep Guardiola anatarajia Alexis Sanchez atabaki Arsenal Januari licha ya kocha huyo wa Manchester City kubashiri kuwa Gabriel Jesus atakuwa nje kwa muda usiopungua miezi miwili.

Nyota huyo wa kimataifa wa Chile, ambaye anaingia kwenye miezi sita ya mwisho kwenye mkataba wake, alihusishwa na tetesi za kutua City mwanzo wa msimu na alikuwa karibu kuondoka Emirates kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Na baada ya Jesus kupata majeraha, Guardiola anatarajia Mbrazili huyo atakuwa nje ya dimba kwa muda wa takribani miezi mwili baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace, Bosi huyo wa zamani wa Barcelona aliukuzwa kama habari hizo zinaweza kumlazimu kumsajili mara moja mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona.

Lakini Guardiola hadhani kama Sanchez ataondoka Arsenal ndani ya wiki chache zijazo.
"Sijui," aliwaambia waandishi alipoulizwa ikiwa Sanchez atakuwa kwenye nafasi nzuri kutua City.

"Ni mchezaji wa Arsenal na nadhani ataendelea kubaki pale. Tutakuwa na mkutano wa ndani na tutaona kipi chema [kwa maana ya uhamisho] , lakini yeye ni mchezaji wa Arsenal na nadhani [atabaki]."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...