Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kwaheri Coutinho

Philippe Coutinho amecheza mechi yake ya mwisho kwa klabu ya Liverpool kwani anatazamia kwenda Barcelona kwa mujibu wa habari
Miamba wa Catalan wamekuwa wakimfukuzia kwa muda mrefu Coutinho lakini walikwama wakiwa wametoa ofa tatu ambazo zilikataliwa kwa ajili ya Mbrazili huyo majira ya joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameweka bayana kuwa alitaka kutua Camp Nou, na kuiomba Reds kumruhusu kuondoka, lakini klabu hiyo ilisisitiza kuwa mchezaji wao nyota haendi popote.
Hata hivyo, Daily Mail limedai kuwa Liverpool imebadili mtazamo na sasa wapo tayari kuachana na mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan, ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Ripoti zinaendelea kudai kuwa ofa isiyopungua £133m tu ndiyo itakayoweza kuishawishi Liverpool kufanya biashara hiyo katika dirisha la uhamisho kipindi hiki kumuuza mchezaji ambaye bado alikuwa muhimu kwao kutokana na kiwango chake matata.
Coutinho amecheza mechi 20 Liverpool katika michuano yote msimu huu, akifunga magoli 12 na kutengeneza mengine tisa zaidi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...