Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Madrid kufanya kufuru ya pesa EPL

Siku hizi kila mahali pesa ndio kila kitu, mwenye pesa anaweza kugeuza kila kitu ndani ya muda mfupi. Hivyo ndio unavyoweza kusema baada ya Florentino Perez kuamua kutangaza vita kubwa sokoni.

Madrid wanaonekana kuyumba sana msimu huu na hakuna matumaini ya kombe lolote huku wapinzani wao Barcelona wakiwa katika msimu bora kuanzia uwanjani na hadi sokoni katika soko hili la usajili.

Sasa Madrid wameamua kujiandaa kulipa kisasi katika manunuzi na kiasi cha £500m kimetengwa kwa ajili ya kufanya usajili wa nyota watatu wakubwa katika dirisha kubwa lijalo la usajili.

£500m yote inaonekana kuelekezwa katika ligi kuu ha Uingereza EPL na kwanza wataanza na Manchester United ambapo watamwaga £100m kwa ajili ya kumsajili golikipa wa Manchester United David De Gea anayetajwa kuwa na thamani zaidi ya £75m.

Madrid hawaishii hapo wanataka kuivamia tena Tottenham Hotspur na wanaamini kiasi cha £200m kinaweza kuwashawishi Tottenham kumuuza mchezaji wao bora kinara wa mabao EPL Harry Kane.

Lakini £200m iliyobaki Madrid watarudi tena Chelsea kuwashawishi kumuuza Eden Hazard ambaye inadaiwa kwamba sio tu kwamba ni kipenzi cha Zinedine Zidane bali hata Florentino Perez anamhusudu Mbelgiji huyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...