Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mohamed Salah ashinda tuzo ya mchezaji bora Afrika

Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kutwaa tuzo ya Mchezaji wa Afrika wa mwaka 2017.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho dhidi ya wachezaji wenzake katika mkutano wa Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika mjini Accra.
Salah, ambaye ataikosa mechi ya Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Everton Ijumaa usiku, amefurahia mwaka wa mafanikio kwa klabu na kwa taifa lake pia.

Baada ya kufunga mara 10 akiwa Roma kati ya Januari na Mei, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aijiunga na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi kwa klabu hiyo na kwa haraka ameshafanikiwa kuweka kimiani magoli 24 katika michuano yote.

Akiongea kuelekea hafla hiyo, Salah aliwaambia waandishi: "Nadhani tuna timu bora ya taifa na tumefanya vizuri kwenye Kombe la Afrika na kufuzu Kombe la Dunia."

Salah pia alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi wa Misri wa 2-1 dhidi ya Congo kufuzu Kombe la Dunia Oktoba kuhakikisha timu yake ya taifa inapata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...