Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Neymar amnyima Cavani kuwa mfungaji bora wa muda wote wa PSG

Neymar alizomewa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon.

Bao la kipindi cha kwanza la Cavani lilimfanya kuwa sawa kwa magoli na mshambuliaji wa zamani Zlatan Ibrahimovic akiwa na magoli 156 katika mashindano yote aliyochezea PSG.

Wenyeji hao waliongoza kwa 4-0 katika kipindi cha kwanza na Neymar alikuwa tayari amekamilisha hat-trick kabla ya PSG kupata penalti.

Hatahivyo raia huyo wa Brazil aliamua kupiga mkwaju huo wa penalti badala ya kumwachia Cavani, hatua iliomfanya Neymar kuzomwa na mashabiki wa timu hiyo , lakini kocha Unai Emery alimtetea mchezaji huyo baada ya mechi hiyo.

'Nadhani Neymar alipiga mkwaju huo wa penalti kwa sababu ilikuwa siku nzuri kwake'', alisema Emery.

''Tunafurahia. Lakini kutakuwa na fursa nyingi kwa Cavani kufunga mabao zaidi''.

Beki wa PSG Thomas Meunier aliitaja hatua hiyo ya Neymar kuwa aibu lakini akaongezea kuwa ni Neymar aliyepewa jukumu la kupiga penalti.

''Angempatia mpira ingekuwa ishara nzuri ya fair Play'', alisema.

''Aliifanyia kazi kubwa timu yetu na swala la kuzomwa na mashabiki , kwa kweli hakuipiga vizuri. Nadhani wachezaji wengi wangefanyiwa hivyo''.

PSG inaongoza kwa pointi 11 kutoka kwa wapinzani wake wa karibu Lyon baada ya mechi 21.

Vionghozi hao wa ligi wameshinda mechi nane zilizopita na michuano ya kuwania mataji, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa sita pekee.

Dijon ambao wako katika nafasi ya 11 katika jedwali hawajashinda hata mechi moja katika mechi nne walizocheza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...