Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ronaldo kafulia au ni mpito tu?

Msimu wa 2005-2006 ulikuwa msimu wa mwisho kwa CR7 kuumaliza akiwa na mabao machache zaidi katika ligi, msimu huo Cristiano Ronaldo alicheza michezo 33 lakini akamaliza akiwa na mabao 9 tu.

Hii leo ni tarehe 15 January 2018 raundi ya pili ya La Liga Cristiano Ronaldo ana mabao 4 tu, tangu ajiunge na Real Madrid hajwahi kufika wakati kama huu akiwa na idadi ndogo ya mabao kiasi hicho.

Msimu wa mwaka 2014/2015 wakati kama huu mwezi wa kwanza tayari CR7 alikuwa ameshacheka na nyavu mara 28 lakini sasa anahangaika na wastani unaonesha anafunga bao moja kila baada ya dakika 311, rekodi mbovu zaidi kwake.

Mbaya zaidi kwa Cr7 hajawahi kuachwa kiasi hichi na mpinzani wake Lioneil Messi kwa idadi ya mabao katika kipindi  kama hiki, Messi ana mabao 16 hadi sasa ikiwa ni tofauti ya mabao 12 na alipo CR7.

Lakini hilo ni La Liga tu ila huko kwingineko katika Champions League kama kawaida yake Mreno huyo anaendeleza uswahiba wake na nyavu ambapo michezo yake 6 ana mabao 9, lakini kwa umri wa sasa wa CR7(33) inaweza kuwa ndio mwisho wa CR7? Tusubiri tuone.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...