Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sanchez akubali kujiunga na Manchester City

Mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza, Alexis Sanchez anatajwa kuwa amekubali kujiunga na klabu ya Manchester City.

Mwandishi mmoja wa habari ambaye ni rafiki mkubwa wa mwanasoka huyo amesema jana kwamba ameambiwa “laivu” na Sanchez kwamba anaondoka rasmi na chaguo lake ni Manchester City.
Gerard Romero ambaye ni mwandishi wa habari raia wa Hispania amesema kwamba ameambiwa na sanchez kwamba anakwenda Man City ili kuungana na kocha wakw wa zamani Pep Guardiola.

Arsenal imekuwa kwa muda mrefu sasa ikihaha kumbakiza mchezaji huyo katika kikosi chake, lakini kwa tarifa hizo mpya ni kama vile jitihada hizo zimekwama.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na msimu bora katika Arsenal chini ya kocha wake, Arsene Wenger na ametumbukiza kambani mabao 30 katika mechi zote za mashindano. Hata hivyo, winga huyo yuko nje ya mkataba msimu ujao na kama anaondoka kwenda Man City maana yake anaondoka akiwa kama mchezaji huru.

Na kwa mujibu wa Romero, tayari mazungumzo ya uhamisho wake yanaweza kuanza wakati wowote ili kujua ni kiasi gani arsenal inaweza kumpa kutokana na muda mdogo wa mkataba wake uliobaki.

Mwandishi huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Alexis Sanchez amekamilisha uhamisho wake kwenda man City. Manchester na Arsenal wameridhia uhamisho wake.”

Wiki iliyopita Sanchez ameiambia Arsenal kwamba hana haraka ya kujadili kuhusu mkataba mpya mpaka baada ya mashindano ya Kombe la mabara. Pep Guardiola amekuwa katika mawindo makali ya kusaka wachezaji wa maana kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...