Klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi Mfaransa Pierre Lechantre, kuwa Kocha mpya atakayekinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa hakina mwalimu baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog mwishoni mwa mwaka jana.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na Mfaransa huyo atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida United leo Januari 18, 2018 katika Uwanja wa Taifa.
Mfaransa huyo alishawahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.
Maoni
Chapisha Maoni