Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez amekubali kwa maneno ya kinywa kujiunga na Manchester City, kwa mujibu wa Marca .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alikaribia kujiunga na City msimu wa majira ya joto na inaonekana anataka kumaliza mkataba wake ambao utaisha mwisho wa msimu huu Emirates.
Inter wanataamani kumsajili kiungo wa Manchester United Juan Mata, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Muhispania huyo atakuwa amemaliza mkataba wake Old Trafford ifikapo mwisho wa msimu huu, ingawa anayo fursa ya kuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja zaidi.
Manchester United wameanza kuhofu kuwa Jose Mourinho anaweza kujiuzulu kazi mwisho wa msimu huu kwa mujibu wa Daily Mail .
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea amekuwa katika kipindi kigumu wiki za hivi karibuni baada ya timu yake kujikuta nyuma ya Manchester City kwa pointi 15 katika mbio za ubingwa na ameweka bayana hadharani kuwa United hawajatumia fedha za kutosha kuwa washindani.
Maoni
Chapisha Maoni