Arsenal wataangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang ikiwa Alexis Sanchez ataondoka uhamisho wa Januari kwa mujibu wa
Gianluca Di Marzio .
Alexis Sanchez bado yupo kwenye rada za Manchester City kwani mkataba wake unazidi kuelekea ukiongoni Emirates.
Na Gunners wameshaanza kufanya mipango ya kutafuta mbadala wake, Aubameyang akipewa kiapumbele.
Kocha mkuu wa Monaco, Leonardo Jardim amesisitiza kuwa Thomas Lemar hataondoka klabuni hapo uhamisho wa Januari.
Mchezaji huyo amekuwa shabaha ya muda mrefu ya Liverpool na Arsenal, lakini Jardim amesisitiza kuwa Lemar hataondoka Monaco hadi majira ya joto.
"Monaco haina tabia ya kuuza wachezaji majira ya baridi. Ni mkakati wetu. Wachezaji wanaelewa na wanafahamu jinsi mambo yanavyokwenda hapa", alisema Jardim.
Manchester City wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 35 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kwa mujibu wa DailyMail.
Maoni
Chapisha Maoni