Mafanikio ya Mohamed Salah mapema msimu huu akiwa Liverpool yameifanya Real Madrid kuvutiwa naye, kwa mujibu wa OK Diario.
Vijana wa Zinedine Zidane wameshindwa kufanya maajabu mbele ya goli na wanatafuta utatuzi wa tatizo hilo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri anapewa nafasi kubwa kutua Bernabeu.
Madrid wanatambua kuwa kukamilika kwa dili hilo kwa uhamisho wa Januari ni vigumu kwa hiyo wanajipanga kwa ajili ya majira ya joto.
Guangzhou Evergrande wamefikia makubaliano na Pierre-Emerick Aubameyang na Borussia Dortmund ya uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon majira ya joto, kwa mujibu wa Sima Sports.
Klabu hiyo ya Chinese Super League italazimika kutoa kitita cha €72 milioni kuhakikish mshambuliaji huyo anatua Beijing, wakiwa wameshatoa dau la €60m.
Meneja w Arsenal, Arsene Wenger hajakataa uwezekano wa Alexis Sanchez kuondoka, na ikiwa mchezaji huyo wa Chile ataondoka kwenda Man City Januari, atakuwa tayari kumsajili Thomas Lemar wa Monaco kuwa mrithi wake, kwa mujibu wa L'Equipe .
The Gunners walishindwa kumsajili Lemar majira ya joto kwa kitita cha £90 ingawa meneja wa Monaco Jardim amesisitiza kuwa Mfaransa huyo hauzwi, lakini Wenger anaweza kufanya jaribio la kumsajili ikiwa Sanchez ataondoka..
Philippe Coutinho yupo tayari kutoa €15m kutoka mfukoni mwke binafsi kuwezesha uhaisho wake kutoka Liverpool kwenda Barcelona, kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Nyota huyo wa Kibrazili ameshakataa ofa nono kutoka Real Madrid na Paris Saint-Germain, moyo wake umeeleke Camp Nou.
Manchester City wanajipanga kutoa dau la £35 milioni kwa ajili ya Alexis Sanchez anayetaka kuondoka Arsenal kwa mujibu wa Daily Mail .
Majeraha ya goti ya Gabriel Jesus yamemlazimu Pep Guardiola kufikiria kumsajilimchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, ambaye amekuwa akivutiwa naye tangu majira ya joto.
Beki wa kati wa Chelsea David Luiz atatolewa kwa mkopo nusu ya pili ya msimu, kwa mujibu wa The Express .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili alipishana kauli na meneja Antonio Conte ambaye sasa anataka kumwondoa Darajani beki huyo mzoefu.
Eden Hazard ameikataa ofa ya pili kusaini mkataba mpya Chelsea kwa mujibu wa RMC .
Mchezji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mkataba wake wa sasa unaishia 2020, lakini Blues wanataka kumpa mkataba zaidi kumzuia kwenda Real Madrid.
Inasadikiw kuwa Antonio Conte amekasirishwa na kitendo cha Hazard kukataa kusaini mkataba mpya, ambao ungemfanya Mbelgiji huyo kuwa mchezaji anayepokea mshahara mnono katika historia ya Chelse.
Man Utd yaanza kum
Manchester United wapo tayari kuuvuruga mchakato wa Real Madrid kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, kwa mujibu wa Don Balon , via the Manchester Evening News .
Maoni
Chapisha Maoni