Jose Mourinho amepania kusimamisha mipango yote kuhakikisha anamsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Griezmann, kwa mujibu wa the Daily Star.
Ingawa mpango ulikuwa kumsajili majira ya joto, lakini baada ya Romelu Lukaku na Zlatan Ibrahimovic kupata majeraha mabadiliko ya haraka yanahitaji kufanyika.
Real Madrid inataka kuachana na mpango wa kuifukuzia saini ya mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, kwa mujibu wa Marca .
Badala yake Zinedine Zidane anajipanga kumpa nafasi kijana wake wa miaka 23 Marco Asensio kwani anamini Mbelgiji huyo ataua maendeleo ya Muhispania huyo.
Mauro Icardi anatamani kutua Manchester United ikiwa ataondoka Inter Milan, kwa mujibu wa Don Balon .
Pamoja na kwamba Icardi amejidhatiti kuisaidia klabu yake katika mbio za taji la Serie A, bado anaangalia mustakabali wake.
Maoni
Chapisha Maoni