Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 3 Januari 2018

Sergio Aguero ametoa dondoo kuwa anaweza kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu.
Goal iliripoti mwezi Desemba kuwa Mwargentina huyo hana furaha katika klabu hiyo msimu huu baada ya kuachwa benchi mara nyingi na Pep Guardiola.
Na ingawa hataki kuondoka, amekiri kuwa klabu ndiyo yenye tamko la mwisho kwenye mustakabali wake.

Philippe Coutinho ameendelea kusisitiza kuwa anataka kuihama Liverpool ili ajiunge na Barcelona Goal imabaini.

Real Madrid wanataka kuvunja mkataba wa Kepa Arrizabalaga ili kuipata saini ya mlinda mlango huyo wa Athletic Club, kwa mujibu wa Marca .
Athletic hata hivyo hawana mpango wa kumuuza kipa huyo wa kimataifa wa Hispania, lakini Mabingwa hao wa Ulaya wanataka kutumia nguvu yao ya mshiko kumpata.

Real Madrid wapo tayari kumuuza Toni Kroos kwa Manchester United ikiwa ni sehemu ya jitihada zao kupata fedha ya kumsajili Neymar kutoka PSG kwa mujibu wa The Express .

West Ham wapo tayari kutoa kitita cha £15 milioni kumsajili Joe Allen kutoka Stoke City, kwa mujibu wa The Daily Mail .
David Moyes anataka kuimarisha safu yake ya kiungo majira ya baridi lakini Stoke City bado hawajawa tayari kumuuza Allen.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...