Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Alexis Sanchez afunga goli lake la kwanza Manchester United

Alexis Sanchez amefunga goli lake la kwanza akiwa na Manchester United baada kushindwa kufanya hivyo katika mechi dhidi ya Tottenham na kufanikiwa kufanya hivyo katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Huddersfield Town.

Wapinzani wao Huddersfield walikuwa wagumu katika kipindi cha kwanza kwani Manchester United walilazimika kusubiri hadi dakika ya 55 ya kipindi cha kwanza walipopata goli kutoka kwa mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Juan Mata.

Dakika ya 68 Manchester United walipata penalti iliyopigwa na Alexis Sanchez ambayo ilitolewa na kipa wa Huddersfield Jonas Lossl.

Hata hivyo haikuchukua dakika nyingi kwa raia huyo wa Chile kufuta makosa yake kwa kupachika kimiani bao katika dakika ya 68.

Hata hivyo Manchester United wataendelea kubaki nyuma ya majirani zao Manchester City kwa jumla ya alama 13.

Maoni