Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Sanchez ahukumiwa miezi 16 jela.

Alexis Sanchez amekubali kifungo cha miezi 16 ya gerezani kwa kufanya udanganyifu wa kodi wakati wake huko Barcelona, ​​ingawa hatatumikia muda jela bado.

Licha ya uamuzi huo, Mchile huyo hawezi kutumia muda gerezani kwa sababu  ni kosa la  kwanza na hukumu ni chini ya miaka miwili.

Mchezaji wa Barcelona Messi alipewa jela la miezi 21 mwaka 2016, lakini aliweza kujitetea kwa faini ya € 250,000.

Alexis alijiunga na Barcelona kutoka Udinese mwaka 2011 na alitumia miaka mitatu akiwa Kikatalani,na kufanikiwa kushinda taji la Liga na Kombe la Dunia ya Club chini ya uongozi wa Pep Guardiola.

Aliondoka kujiunga na Arsenal mwaka wa 2014 na akiwa ni nyota wa timu ya Arsene Wenger mpaka pale alipo hamia Old Trafford Januari katika mpango wa kubadilishana kwa Henrikh Mkhitaryan, licha ya kuwa alionekana angejiunga na Manchester City.

Maoni