Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Bado mechi 12 La Liga imalizike, Madrid kupigania nafasi ya 4.

Jana Real Madrid waliifuata Espanyol katika moja ya michezo ambayo imewashtua watu, Real Madrid walikufabao moja dakika za lala salama goli likiwekwa kimiani na Gerrard Moreno katika dakika ya 92.

Pamoja na Gareth Bale kufikisha michezo 116 katika ligi kuu nchini Hispania idadi ambayo inamfanya kuwa sawa na David Beckham kama Waingereza waliocheza michezo mingi La Liga lakini haikuwa siku nzuri kwao.

Real Madrid sasa wanakuwa na alama 51 ambazo wanakuwa wamezipata katika michezo 26(mchezo mmoja zaidi ya walioko nafasi ya nne), huku Valencia wenyewe wakiwa na alama 49 na mchezo mkononi.

Kwa Madrid ina maana kwamba wamebakisha michezo 12 tu sawa na alama 36 ili kumaliza msimu lakini presha kubwa kwao ni namna walivyopishana na timu ya 4 na hii inawatisha kufika katika nafasi hiyo.

Kwa macho ya kawaida inaonekana Madrid msimu huu wanaweza kupigania nafasi ya nne kwani ndoto za ubingwa zimeshakufa na Champions League ndio sehemu pekee kwao kuweka heshima msimu huu.

Maoni