West Ham iko tayari kumsiani mlinzi wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kwa paundi milioni tatu kutoka kwa West Brom ikifika mwisho wa msimu. (Birmingham Mail)
Kiungo wa Arsenal na timu ya England, Jack Wilshere, 26 anasema atatoka kwenye klabu hiyo kati kati ya mwaka huu, wasipo mpatia mkataba bora zaidi. (Sun)
Manchester United kuachana na mipango ya kuupanua uwanja wa Old Trafford mwaka huu na kujikita zaidi katika kumuunga mkono Jose Mourinho katika kutafuta wachezaji.(Mail)
Winga wa Chelsea kutoka Brazil,Willian,29, anaweza iacha Stamford Bridge katikati ya mwaka na huenda akujiunga na timu ya AC Milan au Manchester United (Star)
Manchester United wameuongeza muda ya mikataba ya viungo Ashley Young, 32, na Daley Blind, 27, na ule wa mlinda mlango Sam Johnstone, 24
Mashetani hao wekundu wana waacha viungo Marouane Fellaini, 30, na Michael Carrick, 36, na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambao watakuwa huru kuondoka na kwa usajili huru majira ya joto.
Alan Pardew atafukuzwa kazi itakapotekea WestBrom watashindwa na Watford Jumamosi. (Mirror)
Nao Juventus wanatamani kumalizia kumsajili kiungo Emre Can, 24, ilikuzuia kuingia kwenye mndada wa kimataifa Ujerumani wakati wa majira ya joto. (La Gazzetta dello Sport)
Liverpool na Barcelona wamevutiwa na kiungo wa Lyon mwenye miaka 19, Houssem Aouar. Kijana huyo Mfaransa amecheza mara 17 kwenye Ligue ya kwanza. (Goal)
Maoni
Chapisha Maoni