ISTANBUL,
Besiktas wamegoma kumalizia dakika 33 zilizobaki za mechi yao ya nusu fainali ya pili ya kombe la ligi dhidi ya Fernabahce iliyoishia kwenye vurugu nzito.
Vurugu hizo zilianza na kwa kocha mkuu wa Besiktas Senol Gunes kurushiwa kiti na kuumia kichwani baada ya fujo zilizotokea baina ya pande hizo mbili.
Shirikisho la soka Uturuki limetoa tamko kwamba mechi hiyo itaendelea ilipoishia Mei 3 bila mashabiki, Besiktas nayo imetoa taarifa ikisema kwamba hawatotokea siku ya mechi wakisisitiza ni wazi wao ndio walikuwa wahanga wa fujo zilizojitokeza.
Mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya timu hizo iliisha kwa sare ya 2-2.
Kwenye nusu fainali nyingine Akhisar Belediyespor imeingia fainali baada ya kuwatembezeshea bakora Galatasaray hivyo wanasubiri mshindi kati ya Besiktas na Fernabahce.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni