Legend wa Barcelona Andres Iniesta ametangaza ataondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika
Iniesta,33, amedumu Barcelona kwa miaka 22 huku akichukua vikombe 31 na timu hiyo.
Ameichezea Barca mechi 669 tangu acheze mechi yake ya kwanza mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 18
Kiungo huyo ametangaza maamuzi hayo leo huku akibubujikwa na machozi mbele ya mkewe,watoto wake na wachezaji wenzake.
Baada ya kuondoka hapo anataraji kujiunga na Chongqing Dangdai inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.
Maoni
Chapisha Maoni