Kiungo mchezeshaji wa Arsenal Mesut Ozil alirushwa kipande cha mkate jana wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya kwanza EUROPA LEAGUE dhidi ya Atletico Madrid na kula kipande cha mkate huo na kuuweka pembeni.
Tumeweza kuona wachezaji kama Dani Alves alivyorushiwa ndizi uwanjani na kuila, sasa tofauti ni kwamba Alves alifanyiwa kama kitendo cha ubaguzi, kwa upande wa mkate bado imeshindikana kutafsiri inamaanisha nini.
Watu wengi wamekuwa wakipinga wachezaji kufanya vitendo kama hivyo kwani haijulikani chakula hicho kimewekewa nini hivyo kuweka hatarini maisha ya mchezaji.
Arsenal watasafiri mpaka Spain Alhamisi ijayo kucheza mechi ya marudiano ndani ya uwanja wa Metropolitano huku Atletico wakiingia na faida ya goli la ugenini.
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
Maoni
Chapisha Maoni