Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ronaldo aweka rekodi UEFA, Sevilla kibarua kigumu dhidi ya Bayern.

Ni Cristiano Ronaldo tena anaendelea kuwanyamazisha wapinzani waReal Madrid, dakika ya 3 tu alipigashuti lake la 9 kwa Gianluigi Buffoon na kufunga baolake la 8 dhidi ya golikipa huyo, hili likiwa baola kwanza katika mchezo huu.
Dakika ya 64 Cristiano Ronaldo tena aliifungia Real Madrid bao la pili na kumfanya kuwa mchezaji katika historia aliyewafunga Juve mabao mengi (9) kabla yaMarcelo kufungia baola 3 Real Madrid.

Hii ni mara ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009 walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu.

Kama hujui tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio baola mapema zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa namabao 38 katikamsimuhuu (michuano yote)ikiwaniidadi kubwa kuliko mchezaji yeyote barani Ulaya.

Tangu klabu ya Juventus wahamie katika uwanja wao mpya mwaka 2011 hawajawahi kupokea kipigo kama hiki katika uwanja huo katika mashindano yoyote yale.

Seville nao almanusra waishangaze Bayern Munich baadaya kupata bao la kuongoza dakika ya 32 kupitia Paulo Sarbia bao linalowafanya Munich kuwa wameruhusu bao katika michezo yao13 ya ugenini katika Champions League.

Lakini Bayern walisawazisha baada ya Jesus Navas kujifunga dakikaya 37 kabla yaThiago Alcantara kuwahakikishia Bayern Munich uhakika waalamatatu muhimu katika ardhi yaugenini.
Ushindi waleo unamfanya kocha wa Bayern MunichJupp Henyckes kuwa kocha wakwanzakatikahistoria kuwahi kushinda michezo12 mfululizo katikamichuano ya Champions League.

Maoni