Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Upepo wa La Liga

Zikiwa zimebaki mechi mbili msimu wa 2017/18 wa La Liga kumalizika, Real Madrid wana pointi 72 na endapo watashinda mechi zao zote wataishia kupata pointi 78 tu.

Msimu wa mwisho Real Madrid kupata pointi chache zaidi kwenye La Liga, ulikuwa msimu wa 2008/09 - ambapo Los Blancos wakiwa chini ya Juande Ramos, hawakushinda taji lolote, wakiwaangalia Barcelona chini ya Pep Guardiola wakishinda mataji matatu na kuwafunga Madrid 6-2 nyumbani kwao Bernabeu. :
Msimu huu mambo yanaweza kuwa tofauti, Madrid wapo kwenye fainali ya ulaya na endapo watashinda watakuwa wamefanikiwa kimataifa lakini watakuwa wamefeli nyumbani tena - mpaka hivi sasa wapo nyuma kwa pointi 18 nyuma ya Wakatalunya ambao tayari wameshabeba ubingwa.

Leo usiku Madrid atakuwa akiumana na Celta Vigo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...