Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Guardiola kuadhibiwa kwa kukiuka sheria za FA dhidi ya Siasa

Shirikisho la soka Soka nchini Uingereza (FA) limemshtaki meneja wa Manchester City juu ya kuvaa kwake Ribbon ya njano  katika miezi ya hivi karibuni.

Guardiola alivaa Ribbon hio ili kuonyesha msaada wake kwa wanaharakati na wafungwa  kisiasa ambao walijitangazia uhuru wa Katalani.

Uhalali wa Ribbon katika soka ya Kiingereza haukuwa na shaka, kama Jose Mourinho aliuliza katika mkutano wa waandishi wa habari mnamo Desemba kama ujumbe huo wa kisiasa unapaswa kuruhusiwa.

Kwa mujibu wa sheria 4.5. ya Sheria ya Mpira wa Kimataifa wa Chama cha Soka (IFAB), wachezaji na makocha haruhusiwi kuvaa vifaa na "slogans yoyote ya kisiasa, kidini au binafsi".

Na FA imeamua kutambua Ribbon ya Guardiola kama uvunjaji wa sheria na itachukua hatua za kumuadhibu kocha wa Manchester City .

"Pep Guardiola ameshtakiwa kwa kuvaa ujumbe wa kisiasa, hasa Ribbon ya njano, kwa ukiukaji wa  kanuni za FA  na matangazo," taarifa kutoka FA inasema.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nitapindua dunia juu chini ili kubaki kama meneja wa Arsenal

Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake. Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal Kazi yake katika timu hiyo iliwekwa utatani wakati alipokataa kudhibitsha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror) Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)

Robert Lewandowski mfungaji bora Bundesliga 2017/2018

Robert Lewandowski amemaliza msimu wa 2017/18 wa Bundesliga akiwa mfungaji bora kwa mara ya 3 kwenye maisha yake ya soka. : • 30 games • 29 goals

Je Barcelona wataweza kuvunja rekodi hizi?

Hadi sasa miamba  ya Catalunya Fc Barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu nchini Hispania na wanaonekana wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kumaliza La Liga bila kupoteza, lakini je na haya yafuatayo wataweza? Magoli 121, Jose Mourinho msimu wa 2011/2012 alimaliza La Liga akiwa na mabao 121, hadi sasa Barcelona wana mabao 70 na itawabidi kufunga mabao 51 katika mechi zao 11 zilizobaki ili kuifikia rekodi ya Mourinho. Zamora award, hii ni tuzo ya kipa aliyefungwa mabao machache, Francisco Liano mlinda lango wa zamani wa klabu ya Sporting Gijon anashikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi La Liga, mabao 18 (1993/1994). Hadi sasa mlinda lango wa Atletico Madrid Jan Oblak ameruhusu mabao 12 katika lango lake huku golikipa wa Barcelona Marc Andre Stegen akiwa ameruhusu mabao 13 hadi sasa, na anasubiriwa kati ya hawa nani atavunja rekodi ya Liano. Real Sociedad record, Barcelona hawajapoteza katika michezo 32 ya La Liga na wamevunja rekodi ya Pep G...